JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Benki ya Absa Tanzania yaongeza kiwango cha mikopo ya watumishi wa umma na kuongeza muda wa marejesho

Share This

 Benki ya Absa Tanzania leo imetangaza maboresho ya huduma yake ya mikopo kwa watumishi wa umma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwapatia watumishi hao unafuu zaidi wa kifedha, urahisi wa kupata huduma na upatikanaji wa mikopo kwa haraka zaidi.

Kupitia maboresho hayo, watumishi wa umma wanaokidhi vigezo sasa wataweza kupata mikopo ya hadi shilingi milioni 300, kutoka milioni 200 za awali, huku muda wa marejesho ukiongezwa kutoka miaka 10 hadi miaka 13. Aidha, Benki imeunganisha mfumo wake wa maombi ya mikopo na mfumo wa Serikali wa Employee Self-Service (ESS), hatua inayowawezesha watumishi wa umma kuwasilisha maombi ya mikopo kwa urahisi zaidi na, kwa kuzingatia vigezo na idhini ya mkopo, kupata fedha ndani ya dakika tano pekee.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo iliyoboreshwa, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere, alisema maboresho hayo yanaakisi dhamira ya Benki ya kukidhi mahitaji ya kifedha ya watumishi wa umma yanayoendelea kubadilika.

“Tunatambua kuwa wateja wetu wana malengo mbalimbali ya kifedha, yakiwemo kuwekeza katika biashara, kujenga nyumba, kusaidia familia zao na kugharamia elimu ya watoto wao. Kwa kuongeza kiwango cha juu cha mkopo hadi shilingi milioni 300, kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 13 na kurahisisha upatikanaji wa mikopo kupitia mfumo wa ESS, tunawapatia watumishi wa umma unyumbufu na urahisi zaidi wa kifedha ili waweze kutimiza mambo yenye umuhimu mkubwa katika maisha yao,” alisema Swere.

Aliongeza kuwa kampeni hiyo imekuja wakati muafaka ambapo Watanzania wanajiandaa na mahitaji ya msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka pamoja na kuanza kwa mwaka mpya wa masomo. Hivyo, aliwahimiza wateja waliopo na wale wanaotarajia kujiunga na Absa kutumia fursa hiyo kunufaika na maboresho hayo ya mikopo.

Kwa upande wake, Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Absa Bank Tanzania, Bw. Beda Biswalo, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano ya Umma wa benki hiyo, alisema kampeni hiyo inaimarisha dhamira ya Benki ya kuwawezesha wateja wake kufikia malengo na matarajio yao.

“Katika Absa, tunaamini kuwa nyuma ya kila lengo la kifedha kuna simulizi binafsi yenye thamani inayostahili kuungwa mkono. Iwe ni mzazi anayewekeza katika elimu ya watoto wake au mtumishi wa umma anayejitahidi kutimiza ndoto yake ya muda mrefu, tunathamini malengo hayo. Huduma hii mpya iliyoboreshwa inadhihirisha ahadi ya chapa yetu isemayo ‘Stori yako Ina Thamani’, sambamba na kuendeleza dhamira yetu ya ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho Pamoja, Hatua Moja baada ya Nyingine.’ Tumejizatiti kufanya huduma za kifedha zipatikane kwa urahisi zaidi ili kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kubadili ndoto na matarajio yao kuwa uhalisia,” alisema Biswalo.

Kupitia kampeni hiyo ya uhamasishaji, Absa Bank Tanzania inawahimiza watumishi wa umma kote nchini kuingia katika mfumo wa Serikali wa ESS, kuchagua Absa Bank Tanzania kama benki wanayoipendelea kwa ajili ya kupata mikopo na kuwasilisha maombi yao ya mkopo.

Watumishi wa umma ambao bado hawajawa wateja wa Absa pia wamealikwa kutumia fursa hiyo, kufahamu zaidi huduma zinazotolewa na Benki hiyo na kujiunga nayo ili kunufaika na huduma hiyo iliyoboreshwa.



Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Maboresha ya Mikopo ya Watumishi wa Umma. Kupitia maboresho hayo, viwango vya mikopo vimepanda kutoka shs milioni 200 hadi milioni 300 na mud awa marejesho umeongezeka kutoka miaka 10 hadi 13. Kulia ni Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bw. Heristraton Genesis.
Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Heristraton Genesis (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Maboresha ya Mikopo ya Watumishi wa Umma. Kupitia maboresho hayo, viwango vya mikopo vimepanda kutoka shs milioni 200 hadi milioni 300 na mud awa marejesho umeongezeka kutoka miaka 10 hadi 13. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Swere na wafanyakazi wengine wa Absa.



Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (waliokaa wa pili kushoto) na Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bw. Heristraton Genesis (Katikati) wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo jijini leo baada ya Uzinduzi wa Maboresha ya Mikopo ya Watumishi wa Umma, jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad