.jpeg)
● Hatua hii inalenga kupunguza changamoto ya mtandao hafifu iliyokuwa ikiwalazimu wananchi kusafiri umbali wa kilomita nane hadi kumi kutafuta huduma za mawasiliano.
LINDI, 16 Novemba 2026. Wakazi wa Kata ya Kiranjeranje, Mkoa wa Lindi, sasa wanaweza kupata huduma za mawasiliano kwa urahisi zaidi kufuatia uzinduzi wa mnara mpya wa Airtel Tanzania, unaolenga kupunguza changamoto ya mtandao hafifu iliyokuwa ikiwalazimu wananchi kusafiri umbali wa kilomita nane hadi kumi kutafuta huduma za mawasiliano.
Mnara huo unatarajiwa kunufaisha takribani wakazi 6,800 katika vijiji vitatu vya Kiranjeranje, Mtandi na Mbwemkuru, kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za simu na intaneti Kila Kona.
Akizungumzia manufaa ya kiuchumi yanayotokana na kuimarika kwa mawasiliano katika eneo hilo, Saleh Safi, Meneja Biashara wa Airtel Mkoa wa Lindi, alisema uwepo wa mnara huo umechangia kufungua fursa za ujasiriamali kwa vijana na kuchochea shughuli za kiuchumi kijijini hapo.
“Baadhi ya vijana wameanza kujipatia kipato kupitia shughuli zinazotegemea mawasiliano, zikiwemo huduma za bodaboda na usajili wa laini za simu, huku wengine ambao awali hawakuwa na ajira sasa wakipata kipato cha kila mwezi kupitia huduma za matandao wa simu wa Airtel” alisema.
Safi aliongeza kuwa Kiranjeranje ni eneo lenye machimbo makubwa ya gypsum yanayovutia watu kutoka maeneo mbalimbali nchini. Na upatikanaji wa mtandao unarahisisha mawasiliano na matumizi ya huduma za kifedha kwa wageni, wafanyabiashara na wakazi, hivyo kusaidia shughuli za biashara na miamala kuendelea kwa urahisi zaidi.
Akizungumzia mabadiliko yanayotarajiwa kutokana na uwekezaji huo, Ablemani Simba, Diwani wa Kata ya Kiranjeranje, alisema awali wakazi walikabiliwa na changamoto ya mtandao hafifu, hali iliyowalazimu kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za mawasiliano.
“Awali mtandao haukuwa mzuri na wananchi walilazimika kusafiri umbali wa kilomita nane hadi kumi kutafuta huduma za mawasiliano. Baada ya kufungwa kwa mnara huu, mawasiliano yameimarika na wananchi sasa wanaweza kupata huduma za mawasiliano na kifedha kwa urahisi zaidi”
Mbali na hilo, Mnara huo unatarajia kunufaisha vijiji vitatu vya Kiranjeranje, Mtandi na Mbwemkuru, vyenye jumla ya wakazi takribani 6,800.
Kwa upande wake, Lameck Darema, ambaye anatoa huduma za kifedha katika eneo hilo, alisema kabla ya mnara huo kujengwa, upatikanaji mdogo wa mtandao wa Airtel uliwafanya baadhi ya wakazi kutumia mitandao mingine kutuma na kutoa fedha, hali iliyopunguza idadi ya wateja na kamisheni kwa mawakala.
Alisema hali imebadilika baada ya mnara huo kuanza kutoa huduma, huku upatikanaji bora wa mtandao ukisaidia kuvutia wateja wengi zaidi wa Airtel na kuongeza kipato cha mawakala kupitia kamisheni.
Akielezea furaha ya wakazi kufuatia kuimarika kwa mawasiliano, Latifa Makele, mkazi wa Kijiji cha Kiranjeranje, alisema ujio wa mnara huo ni faraja kubwa kwa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya mawasiliano bila kuwa na uhakika wa lini wangepata suluhisho.
“Ujio wa mnara huu ni zawadi kubwa kwetu wananchi. Tumekuwa tukikabiliwa na changamoto za mawasiliano kwa muda mrefu bila kujua ni lini hali ingebadilika. Tunaishukuru Airtel kwa hatua hii na tunafurahia kupatikana kwa huduma hizi katika eneo letu. Tuna matumaini kuwa tutaendelea kunufaika na maboresho ya mawasiliano,” alisema Makele.
Ukuaji wa matumizi ya huduma za mawasiliano kwa njia ya simu nchini unaonesha umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya mawasiliano katika jamii zilizo nje ya miji mikubwa. Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa idadi ya usajili wa laini za simu nchini ilifikia milioni 117 Juni 2026, ikiwakilisha ongezeko la asilimia 4.51 ikilinganishwa na Machi 2026.
Uzinduzi wa mnara wa Airtel Kiranjeranje unaonesha dhamira ya Airtel Tanzania ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za mawasiliano na fursa za kidijitali kwa jamii nyingi zaidi nchini.
Kupitia uwekezaji endelevu katika mtandao wake, Airtel Tanzania inaendelea kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi, wafanyabiashara na wajasiriamali Kila Kona.


No comments:
Post a Comment