Na Mwandishi wetu, Mkuranga
WAREMBO watachuana katikafainali za kumpata Mrembo wa Kanda ya Mashariki Novemba 6 , 2026 shindano lililopangwa kufanyima Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi wa Miss Eastern Zone Yusuf Hassan amesema mrembo atavikwa taji atapata zawadi ya gari na tiketi ya kushiriki fainali za kumpata Miss Tanzania 2026.
Kambi ya warembo itakuwa boza katika kisiwacha Kuruti kilichopo Mkuranga zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washiriki wengine.
Mkurugenzi Yusuph amesema hayo leo tarehe 27 Oktoba 2026 alipozungumza na Waandishi wa Habari Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Amesema warembo hao wanatarajiwa kuungia kambini hivi karibuni ambapo watatumia usafiri wa bahari wakitokea Sea Cliff Masaki Jijini Dar es Salaam na kwenda hadi Kisiwa cha Vikuruti kilichopi Mkuranga.
Mkurugenzi Yusuph ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Idara ya Utamaduni na Michezo na kuhakikisha vijana wanafaidika na mikopo ya makundi maalumu.
Aidha shukrani zingine zimfikie Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo kutokana na maelekezo aliyowapatia pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga.
Wasanii nyota mbalimbali wanatarajia kutumbuiza akiwemo msanii wa Lebo ya WCB D-Voice ,Isha Mashauzi,Yammy Tz ,Dogo Parten, wasanii wazawa wa Mkuranga na Mkoa wa Pwani Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheriakwa ujumla na wengine wengi .
Amesema anamshkuru mdau mkubwa wa shindano hilo BOSS BOSS, Adey na wengine wengi.
Amesema tayari wameanza kuuza tiketi ambapo zinapatikana kwa njia ya mtandao na kawaida zinazouzwa kwa shilingi 20,000, 50,000 (VIP) na 100,000 (VVIP) tiketi hizo zinauzwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Mkuranga na ofisi zote za utamaduni Mkoani hapa.
Sehemu zingine zinazouzwa tiketi hizo ni Parachichi,BOSSBOSS Vikindu na Samaki Sport Morogoro.




No comments:
Post a Comment