Waziri wa Kazi na Kinga ya Jamii wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. Alfred Mutua, EGH (katikati), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue, jijini Dar es Salaam, Oktoba 6, 2026.
Tanzania inatarajia kupata fursa zaidi za ajira katika nchi za Ghuba, zikiwemo nafasi za kitaalamu kwa madaktari, wauguzi, wafamasia na wahandisi, kufuatia Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira.Katika mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Tanzania imepata fursa ya kuimarisha ushirikiano na nchi za Ghuba pamoja na mataifa mengine ya Afrika katika kukuza fursa za ajira na kurahisisha uhamaji wa wafanyakazi.



No comments:
Post a Comment