Taharuki imetanda katika Kitongoji cha Saburi, kilichopo Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, kufuatia mgogoro wa ardhi unaohusisha wananchi na mwekezaji anayedaiwa kutaka kubomoa makazi yao.
Wananchi wameeleza kwa uchungu hali wanayopitia kutokana na mgogoro huo, wakidai kuwa kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi, likiambatana na tingatinga, lilifika eneo hilo kwa lengo la kubomoa nyumba zao.
Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi hao, baadhi yao walijitokeza kuzuia zoezi hilo, hali iliyofanya kukamatwa kwa baadhi ya wakazi ambao wanadaiwa kushikiliwa mahabusu kwa zaidi ya siku 20 bila kufikishwa mahakamani.
Aidha, baadhi ya wananchi wanadaiwa kuishi mafichoni kutokana na hofu ya kukamatwa, huku familia zikiendelea kukabiliwa na sintofahamu kuhusu usalama wa makazi yao na hatima ya mgogoro huo.
Wananchi hao wanaiomba Serikali na mamlaka husika kuingilia kati ili kuchunguza madai hayo, kuhakikisha haki inatendeka na kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo bila kuhatarisha maisha na makazi yao.








No comments:
Post a Comment