JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RC Msengi aunga mkono kampeni ya NMB, ataka elimu kwa wakulima

Share This

Benki ya NMB kwa kushirikiana na CMC Agri Limited imezindua kampeni ya Korosho Yangu, Benki Yangu mkoani Mtwara, itakayowezesha vyama vikuu vitano vya ushirika kushindania matrekta, AMCOS kushindania pikipiki na wakulima mmoja mmoja kupata fursa ya zawadi za fedha kwa kuongeza amana benki katika msimu wa korosho wa 2026/2027.

Akizindua kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi, amesema matrekta hayo yanaweza kusaidia kupunguza changamoto za usafirishaji wa pembejeo na korosho katika maeneo yenye miundombinu duni. Ameitaka NMB kutoa elimu kuhusu masharti ya kampeni na mikopo, huku akiishauri kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wakulima kupata mikopo ya kulipia bima ya afya kabla ya mavuno.

Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa NMB, Nsolo Mlozi, amesema matrekta hayo yatawezesha usafirishaji wa korosho, kunyunyizia dawa na maandalizi ya mashamba, huku washindi wakipatikana kwa kuzingatia kiwango cha amana, miamala na masharti ya kampeni.

Meneja wa CMC Agri Limited Tanzania, Stuart Leishman, amesema matumizi ya zana za kisasa ni muhimu kuongeza tija ya kilimo, huku Mwenyekiti wa MAMCU, Alhaji Azam Mfaume, akieleza kuwa kampeni hiyo itachochea ushindani wa vyama vya ushirika katika kuongeza amana na kuwasaidia wakulima kupata huduma bora za kilimo.










No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad