JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

Share This

-WAZINDUA MIRADI YA ELIMU, AFYA NA MIUNDOMBINU

-MAAFISA USAFIRISHAJI WACHANGAMKIA FURSA ZA HIFADHI SKIMU IKIWEMO MAFAO YA MATIBABU

Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chachu ya maendeleo nchini baada ya kumulika na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Kwela, Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa kulinda amani kama msingi wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Katika ziara yake iliyofika katika Kata ya Laela, Mwenge wa Uhuru umekagua na kuzindua miradi inayohusisha sekta za elimu, afya na miundombinu, ikiwemo shule ya sekondari, zahanati na daraja, sambamba na shughuli za ujenzi wa barabara.

Miradi hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kuboresha mazingira ya wananchi katika jimbo hilo, huku Mwenge wa Uhuru ukiendelea kutekeleza jukumu lake la kuhamasisha uwajibikaji, mshikamano na maendeleo yanayomgusa mwananchi moja kwa moja. Akizungumza Oktoba 10, 2026, katika Kata ya Laela, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni miongoni mwa matokeo ya mazingira ya amani yaliyopo nchini.

Mwang’onda amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuendelea kuitunza na kuilinda amani, akisisitiza kuwa maendeleo endelevu yanahitaji utulivu, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Rukwa, hususan Jimbo la Kwela.

















Sangu amesema miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru ina umuhimu mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo, akieleza kuwa utekelezaji wake unatarajiwa kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya eneo hilo.



Katika hatua nyengine Mhe. Sangu ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) kwa kuendelea kuyafikia makundi mbalimbali ya vijana waliojiari wakiwemo madereva boda boda zaidi ya 1900 ambapo NSSF iliwapa elimu ya Hifadhi ya Jamii na kuwasajili kuwa wanachama kupitia mpango wa Hifadhi Skimu.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad