Na Mwandishi Wetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imeibuka kidedea na kutwaa ushindi wa kitaifa katika Maonyesho ya Wiki ya Chakula na Lishe Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Usagara, jijini Tanga. Ushindi huo umetokana na maandalizi mazuri na juhudi za kuunga mkono wakulima wadogo kwa kuwapatia fursa za kujifunza teknolojia mpya za kilimo, kuongeza thamani ya mazao na kuonesha bidhaa zao zenye ubora.
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Naima Chondo, amesema halmashauri hiyo imeonesha mnyororo mzima wa kilimo, kuanzia uzalishaji shambani hadi bidhaa zinapofikishwa sokoni. Ameongeza kuwa ushindi huo ni chachu ya kuendelea kuwawezesha wakulima na kuimarisha sekta ya kilimo, huku akiwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika kilimo na biashara kutokana na uwepo wa ardhi yenye rutuba inayofaa kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Ayubu Sebabili, amesema wilaya hiyo imejipanga kuimarisha elimu ya lishe kwa wananchi na wanafunzi wa shule kwa kuhamasisha ulaji wa mlo kamili na matumizi sahihi ya chakula ili kupunguza tabia ya kutupa chakula. Amesisitiza kuwa lishe bora ni msingi wa ukuaji, maendeleo na afya njema, hivyo elimu hiyo ni muhimu katika kujenga jamii yenye afya na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa chakula chenye virutubisho vya kutosha.
Sebabili amesema Muheza ni miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa za kilimo cha mazao mchanganyiko, yakiwemo mahindi, ndizi na mazao ya viungo kama karafuu, iliki na mdalasini. Ameeleza kuwa mazao hayo yana fursa nzuri katika masoko ya ndani na kimataifa, huku wilaya hiyo ikitenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo cha kisasa na ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani na kipato cha wakulima.
Amesema wilaya hiyo pia inatarajia kufanya kongamano kubwa la wadau wa kilimo litakalowakutanisha wakulima, wafanyabiashara, taasisi za fedha na wawekezaji kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja kuelekea msimu ujao wa kilimo. Ameongeza kuwa uwepo wa ardhi yenye rutuba na mvua zinazosaidia shughuli za kilimo ni fursa muhimu kwa wawekezaji, huku viongozi wa wilaya wakiwa tayari kutoa ushirikiano katika kuwezesha miradi ya kilimo na biashara.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Buriani, amewapongeza washiriki na washindi kwa kuonesha ubunifu na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa wakulima na wananchi waliohudhuria maonyesho hayo. Amesema Mkoa wa Tanga una fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na uwepo wa Bandari ya Tanga inayopanuliwa, Bomba la Mafuta na uwekezaji katika sekta za kilimo na viwanda, hivyo amewahimiza wawekezaji kutumia fursa hizo kuimarisha uzalishaji wa chakula na kukuza uchumi.
Dkt. Buriani amesema Serikali ya Mkoa wa Tanga imejipanga kupokea wawekezaji katika sekta ya kilimo, akibainisha kuwa hatua zinazochukuliwa zinaendana na juhudi za kufikia Lengo la Pili la Maendeleo Endelevu la Umoja wa Mataifa la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030. Pia ametoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Shirika la Chakula Duniani (WFP) na wadau wengine kwa kushiriki katika maonyesho hayo na kuunga mkono juhudi za kuimarisha uzalishaji wa chakula na lishe bora.
Maonyesho hayo yamehitimishwa jijini Tanga yakiwa na kaulimbiu isemayo “Ubunifu wa Leo, Lishe Bora ya Kesho, Kuelekea Dira 2050,” yakilenga kuhamasisha ubunifu katika uzalishaji wa chakula, matumizi bora ya mazao na kuimarisha lishe kwa jamii. Maadhimisho hayo pia yametoa fursa kwa wakulima, wadau wa kilimo na wawekezaji kubadilishana uzoefu, kujifunza teknolojia mpya na kutambua fursa za kuongeza thamani ya mazao kwa manufaa ya wakulima na uchumi wa taifa.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

No comments:
Post a Comment