
.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za usafi katika Mto Ng’ombe Jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2026, kutekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi aliyoyatoa wakati wa ziara yake Septemba 18, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akishiriki zoezi la kufanya usafi kwa kutumia mashine maalum katika Soko la Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (mwenye kofia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo wakati wa akikagua shughuli za uhifadhi wa mazingira Mto Msimbazi, Kata ya Kipawa, Mtaa wa Karakata Jijin Dar es Salaa, Septemba 3, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akikagua shughuli za usafi katika Mto Ng’ombe Jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2026, kutekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi aliyoyatoa wakati wa ziara yake Septemba 18, 2026.
PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
NA; MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi hasa pembezoni mwa Mto Msimbazi kuhama kwa kuwa wanahatarisha usalama wa maisha yao na mali.
Waziri Masauni amesema ni bora kwa sasa wakatafuta makazi mbadala kwa kuwa mazingira wanayoishi sio salama kwao pamoja na familia zao hasa kutokana na utabiri uliotolewa kwa uwepo wa El Nino.
Mhe. Masauni ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2026, kutekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi aliyoyatoa wakati wa ziara yake Septemba 18, 2026.
“Kwa kweli Maisha yao yapo hatarini, niendelee kutoa wito kwa wananchi wote ambao wanaishi katika maeneo kama haya, sio kwa Dar es Salaam pekee bali nchi nzima wanapaswa kuchukua tahadhari juu ya hii.
“Nipende kusisitiza kwa watu wote kusikiliza maelekezo ya wataalamu hasa katika kipindi hiki juu ya utaratibu wa kuishi katika maeneo haya au ikiwezekana kuhama na kutafuta makazi mengine,” amesema Masauni.
Aidha, Waziri Masauni amesema kuwa licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kukabiliana na changamoto ya taka na uchafu katika mifereji na mito, baadhi ya wananchi bado wanaendelea kutupa taka katika maeneo hayo.
Ameongeza kwa kuwataka viongozi katika ngazi zote kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kila mmoja anapaswa kuwajibika ili kuhakikisha maelekezo yanatekelezeka kwa kuhakikisha miji inakuwa misafi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha mifereji na njia za maji zinakuwa safi na zinaweza kupitisha maji kwa ufanisi wakati wa mvua.
Ameongeza kuwa Halmashauri itaendelea kushirikisha sekta binafsi katika huduma za usafi, huku Dampo la Pugu Kinyamwezi likipokea excavator mpya ili kuongeza ufanisi wa usimamizi wa taka.


.jpg)






No comments:
Post a Comment