JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Elimu ya menopause yawataka wanawake na wanaume

Share This
Mtumishi wa Mungu, Isaac Paul Hammoud (IPM) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2016.
Mkurugenzi wa PEMA Event, Khairat Ndassiwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2016.

Na Mwandishi Wetu
PEMA Event kwa kushirikiana na MS One Agency wameandaa tukio maalumu la kutoa elimu kuhusu mabadiliko ya mwili na homoni yanayotokea wakati wa premenopause, menopause na postmenopause, wakilenga kuongeza uelewa kwa wanawake, wanaume na Wanandoa nchini Tanzania na kuondoa hofu pamoja na imani potofu zinazohusishwa na hatua hizo za maisha.

Wadau hao wamesema ukosefu wa elimu kuhusu mabadiliko hayo umekuwa ukisababisha baadhi ya wanawake kuishi kwa hofu, huku wengine wakihusisha hali wanazopitia na kulogwa, kuingiliwa au maradhi mengine badala ya kutafuta elimu na ushauri sahihi wa kitaalamu.

Akizungumza leo, Oktoba 12, 2026, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa PEMA Event, Khairat Ndassiwa, amesema tukio hilo litafanyika Oktoba 31, mwaka huu, katika ukumbi wa ghorofa wa Golden Jubilee, jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuelimisha jamii kuhusu menopause na changamoto zinazowakabili wanawake katika hatua hiyo ya maisha.

Amesema tukio hilo ni sehemu ya juhudi za PEMA Event kwa kushirikiana na MS One Agency kuhamasisha mazungumzo ya wazi kuhusu masuala ambayo bado hayajaeleweka ipasavyo katika jamii, huku wanawake wakipewa nafasi ya kueleza uzoefu wao na kupata ushauri unaofaa.

Kwa upande wake, Mtumishi wa Mungu, Isaac Paul Hammoud (IPM), amesema jamii inapaswa kutambua umuhimu wa elimu kuhusu masuala ya maisha na afya badala ya kuyatafsiri kwa mitazamo isiyo sahihi.

“Elimu haina mwisho. Usifanye unajua kila kitu, bado unajifunza,” amesema IPM, akisisitiza kuwa elimu kuhusu menopause inapaswa kuwahusisha wanawake na wanaume kwa kuwa wote ni sehemu ya familia na jamii.

Amesema wanaume wana nafasi muhimu ya kuwasaidia wanawake wanaopitia mabadiliko hayo, hivyo wanapaswa kupata uelewa utakaowawezesha kutoa msaada unaohitajika. Amewahimiza wananchi, hususan wakazi wa Dar es Salaam, kushiriki katika tukio hilo ili kupata maarifa yatakayowasaidia kuelewa menopause na changamoto zake.

Naye Mkurugenzi Mwenza wa PEMA Event, Imelda Mtema, amesema elimu kuhusu mabadiliko ya homoni kwa wanawake ni muhimu katika kuwasaidia kuelewa kinachoendelea katika miili yao na namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo.

Amesema baadhi ya wanawake hukosa uelewa wa kutosha kuhusu vipindi vya premenopause, menopause na postmenopause, hali inayoweza kuwafanya kudhani kuwa wana magonjwa mengine au kuhusisha mabadiliko hayo na imani potofu.

Mtema amesema kupitia tukio hilo, PEMA Event kwa kushirikiana na MS One Agency wanalenga kujenga uelewa mpana kwa wanawake, wanafamilia, waajiri na jamii kwa ujumla ili kuwapa wanawake wanaopitia mabadiliko hayo heshima, uelewa na msaada unaostahili.

Amesisitiza kuwa ni muhimu jamii kutafuta maarifa mapema badala ya kusubiri changamoto zitokee, akieleza kuwa tukio la Oktoba 31 litatoa nafasi kwa wanawake na wanaume kujifunza, kuzungumza na kubadilishana uzoefu kuhusu menopause na masuala yanayohusiana nayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad