WAZIRI wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amefanya mkutano na Wadau wa Tasnia ya Tumbaku mkoani Tabora tarehe 3 Oktoba 2026 kutatuai changamoto za tasnia hiyo kuanzia ya bei ya pembejeo, masoko, teknolojia duni ya ukaushaji pamoja na madeni ya AMCOS na halmashauri ambayo hayajalipwa kwa wakati.
Kikao hicho kimewahusisha wakulima; Vyama vya Msingi (AMCOS); wanunuzi pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania; ambapo Mhe. Chongolo amezitaka kampuni zinazodaiwa fedha za wakulima kuhakikisha malipo yote yamekamilika ifikapo tarehe 30 Oktoba 2026, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuchelewesha malipo baada ya wakulima kuuza Tumbaku.
Kuhusu bei ya pembejeo, Mhe. Chongolo amesema Serikali imechelewesha kutangaza bei kwa makusudi ili kutafuta unafuu kwa wakulima. Ameelekeza kufanyika mazungumzo ya wadau ndani ya siku kumi (10) ili kupata bei nafuu zaidi, huku akisisitiza kuwa mbolea lazima isambazwe kwa wakulima ndani ya wiki mbili.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Dkt. Gerald Mongella, amesema kuwa uchumi wa mkoa huo unategemea zao la Tumbaku huku akisisiriza Serikali kuongeza kiwango cha ruzuku kwa wakulima wa Tumbaku na kuharakisha mchakato wa kuanzishwa kwa kiwanda cha mbolea mkoani Tabora unafanikishwa ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Nae Meneja wa Bodi ya Tumbaku Kanda ya Tabora, Bw. Albert Charles amesema kuwa licha ya changamoto zilizopo, idadi ya wanunuzi imeongezeka kutoka kampuni tatu msimu wa 2020/2021 hadi kufikia kampuni 18 kwa sasa, hatua inayotoa matumaini kwa wakulima.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)


No comments:
Post a Comment