Kama Muandaaji wa Kimkakati wa Jukwaa la Uwekezaji Tanzania 2026 (Tanzania Investment Forum 2026), Benki ya NMB itakua Uingereza kuungana na wawekezaji wa kimataifa, watunga sera na viongozi wakuu wa biashara kujadili fursa za uwekezaji nchini Tanzania.
Benki ya NMB itawakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi, David Nchimbi; Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna, Mkurugenzi wa Bodi na Afisa Mkuu wa Fedha, Juma Kimori pamoja na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Uwekezaji, Uendelevu na Mawasiliano, Innocent Yonazi.
Katika jukwaa hili, Benki ya NMB ikishirikiana kwa Karibu na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza itatoa mawasilisho yanayolenga kuhamasisha mtaji, kufungua fursa za uwekezaji na kujenga ubia wenye matokeo chanya huku wakielezea nafasi ya sekta ya fedha katika kuharakisha ukuaji endelevu wa Tanzania.
Kwa wawekezaji wa kimataifa, Tanzania iko tayari kwa Mitaji kupitia Uwekezaji, ubia na biashara.
Wakiwa London, watajadili fursa zitakazo ongoza safari ya uwekezaji Tanzania.
Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji lakini Benki ya Nmb ipo tayari kushirikiana kibiashara na wawekezaji wanaotaka kuwekeza Tanzania.
Tags
# BIASHARA
Share This
Jiachie Blog
BIASHARA
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.



No comments:
Post a Comment