
Na Mwandishi Wetu
WAHITIMU wa Shule ya Msingi na awali ya Pius Pre and Primary school wametakiwa kuendelea kuwa na tabia njema baada ya kupatiwa malezi mazuri Shuleni hapo.
Akizungumza jana katika mahafali yaliyofanyika shuleni hapo Mwalimu Mkuu Sospeter Simon Mabanga amesema Mabanga nendeni mkawe chachu ya maendeleo katika jamii zenu kwani elimu mlizopewa hapa shuleni ni hazina katika familia na taifa kwa ujumla.
Aidha Mabanga ametoa shukrani kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuruhususekta binafsi kutoa elimu hapa nchini.
Katika mahafali hayo mgeni rasmi alikuwa Dkt. Mwamba Ally Jingu ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Uhasibu (IFM) ambaye ametoa pongezi kwa uongozi pamoja wa wafanyakazi wote kwa kuwasiamia vema wanafunzi hao
Wakati huohuo zawadi za fedha zimetolewa kwa waalimu ikiwa ni mikakati ya kuinua taaluma na utoaji motisha kwa waalimu kutokana na namna walivyofaulisha kwenye mitihani yao ya taifa.
Shule hiyo ya Pius Pre and Primary iko Kongowe Jijini Dar es Salaam.
.jpeg)


No comments:
Post a Comment