JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


VIONGOZI WA ULINZI CHADEMA WAREJEA CCM

Share This

 Na Mwandishi Wetu


VIONGOZI nane waliokuwa wakihusika na masuala ya ulinzi na usalama katika ngazi mbalimbali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa viongozi hao ni aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA Taifa, Prosper Makonya, ambaye anatajwa kushika nafasi hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa Kiongozi wa Idara hiyo, Ali Kibao.

Wanachama hao wamepokelewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, ambaye aliwaongoza kula kiapo kwa kusoma ahadi za wanachama zilizowekwa katika Katiba ya CCM.

Wengine waliojiunga na CCM ni aliyekuwa Mkuu wa Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza, Peter Mashauri; aliyekuwa Mkuu wa Ulinzi na Usalama Jimbo la Kawe, Gibson Mwamaliga; na aliyekuwa Mkuu wa Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tanga, Simon Lukindo.

Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Ulinzi na Usalama Jimbo la Korogwe, Sarafu Jengo; aliyekuwa Mkuu wa Ulinzi na Usalama Lushoto, Samwel Sylvester; pamoja na viongozi wengine waliowahi kushika nafasi za ulinzi na usalama katika mikoa ya Simiyu na Morogoro.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Makonya, ambaye baada ya kuondoka CHADEMA alijiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), alisema ameamua kujiunga na CCM kwa sababu anaamini ni chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi na kuyasimamia.

“Ndani ya CCM kuna kila aina ya watu, na ninaweza nikadiriki kusema Chama Cha Mapinduzi ni chama cha Watanzania. Ndani ya CCM kuna maamuzi, wengine wanafuata njia za watu,” alisema.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad