Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Dar es Salaam, TRAMEPRO limesema changamoto hizo zinaweza kupunguza uwezo wa mashirika kutekeleza shughuli zao, kuwafikia walengwa na kuhakikisha uendelevu wa miradi yao.
TRAMEPRO limependekeza Serikali na wadau wa maendeleo kuongeza fursa za ruzuku kwa mashirika yenye miradi yenye tija, huku NGOs zikitakiwa kujenga mifumo endelevu ya mapato kupitia wanachama, ubia na shughuli halali za uzalishaji mali.
Aidha, shirika hilo limependekeza kuimarishwa kwa mafunzo katika maeneo ya uandishi wa miradi, usimamizi wa fedha, utawala bora, matumizi ya teknolojia na ufuatiliaji wa matokeo.
TRAMEPRO pia limeitaka Jukwaa la NGOs Mkoa wa Dar es Salaam kuimarisha ushirikiano kati ya mashirika, Serikali, sekta binafsi na taasisi za utafiti, pamoja na kuongeza ushiriki wa NGOs katika mipango ya maendeleo ya Serikali za Mitaa.
Shirika hilo limesisitiza kuwa uendelevu wa NGOs hauhitaji fedha pekee, bali pia uongozi bora, uwajibikaji, ushirikiano na uwezo wa kuonesha matokeo yanayopatikana kwa wananchi.
Imetolewa na: Boniventura Mwalongo, Katibu Mkuu wa TRAMEPRO.



No comments:
Post a Comment