JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TAREWU, TIB Rasimali Zasaini Makubalino Katika Elimu ya Fedha na Uwekezaji

Share This

 

Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi wa Wakusanya Mapato nchini (TAREWU) Dkt. Michael Marere na Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Rasilimali wakionesha hati ya makubaliano baada ya kukubalino.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Rasilimali Brighton Kinemo pamoja na Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi wa Wakusanya Mapato Tanzania (TAREWU) wakisaini hati ya makubaliano ya TIB kutoa elimu ya fedha na uwekezaji kwa wanachama wa (TAREWU).
Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Rasilimali , Brighton Kinemo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makubaliano kati ya Taasisi yao na Chama cha Wafanyakazi wa Wakusanya Mapato (TAREWU) kushoto ni Katibu wa Chama hicho Dkt. Michael Marere.

WAKATI kukiwa kuna ombwe la elimu ya fedha na uwekezaji nchini. Chama cha Wafanyakazi wa Wakusanya Mapato (TAREWU), na TIB Rasilimali zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika elimu ya fedha na uwekezaji.

Makubaliano hayo yamekiwa leo Septemba 14, 2026 jijini Dar es Salaam, ambapo imeeelezwa kuwa makubaliano hayo ni mwanzo wa utekelezaji.

Brighton Kinemo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, wakati wa makubaliano hayo amesema kuwa utekelezaji wa mkataba huo utawawezesha wafanyakazi wa TAREWU kupata elimu ya fedha na uwekezaji itakayowawezesha kujimarisha kiuchumi kabla na baada ya kustaafu.

"Mtu anaweza kufanya kazi kwa miaka mingi lakini suala la msingi una elimu gani ya fedha na uwekezaji,".

"Kustaafu kunaandaliwa mapema. Makubaliano tunayokubaliana leo sio mwisho ni mwanzo wa utekelezaji,"

Naye Dkt. Michael Marere, Katibu Mkuu wa TAREWU amesema kuwa elimu ya fedha na uwekezaji kwa wanachama wake kupitia TIB itawawezesha wanachama wake kupaya elimu hiyo.

“Ustawi wa mwanachama hauishii katika masuala ya maslahi ya kikazi pekee. Tunaamini kwamba mwanachama anayekuwa na maarifa sahihi ya fedha, uwezo wa kupanga na kusimamia kipato chake, pamoja na kufanya maamuzi sahihi ya kifedha, anakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kujenga maisha yenye ustawi na usalama wa kiuchumi.”

Dkt. Marere ameongeza:“Hii ndiyo sababu TAREWU imeweka elimu ya fedha na ustawi wa kiuchumi kuwa miongoni mwa vipaumbele muhimu katika Mpango Mkakati wetu wa Pili wa 2026–2030. Ushirikiano wetu na TIB Rasilimali ni hatua ya kimkakati ya kuhakikisha kwamba azma hii inatekelezwa kwa vitendo na kuleta manufaa yanayoonekana katika maisha ya wanachama wetu.”

Aidha, Katibu Mkuu huyo amesisitiza kuwa TAREWU inalenga kujenga utamaduni wa “mwanachama mwenye maarifa, mwenye uwezo wa kifedha na mwenye ustawi”, akieleza kuwa elimu ya fedha inapaswa kuwa sehemu ya uwezeshaji endelevu wa wanachama katika hatua mbalimbali za maisha yao.

“Tunataka kuondoka kwenye mtazamo wa elimu ya fedha kama tukio la mara moja na badala yake kuijenga kama utamaduni endelevu ndani ya TAREWU. Lengo letu ni kuwawezesha wanachama kuelewa fedha zao, kuzipangia malengo, kujenga akiba, kuwekeza kwa uelewa na kufanya maamuzi yanayolinda ustawi wao wa sasa na wa baadaye.”

Wakati huo huo Dkt. Marere amesema TAREWU hivi karibuni itazindua mfuko wa pamoja na uwezeshaji kwa wanachama wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad