NA MWANDISHI WETU
TIMU ya wanawake ya mchezo wa Hockey ya Royal Queens kutoka Zanzibar, imeanza kujiandaa na michuano ya Mapinduzi Cup inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani ambapo imefanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wa mchezo hao Tanzania Bara.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Hockey Zanzibar , Juma Hassan Juma,amesema ni kwa mara ya kwanza timu ya Hockey ya wanawake kutoka Zanzibar kutua jijini humo kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wa mchezo huo Tanzania bara.
Amesema , mazoezi hayo ya wiki moja yamekuwa na ufanisi mkubwa katika kuwanoa wachezaji wa timu hiyo ya wanawake.
"Tunaahidi kufanya vizuri katika michuano ya Mapinduzi Cup inayotarajiwa kufanyika Januari mwakani,"amesema Juma.
Ameeleza, changamoto iliyokuwepo awali Zanzibar ni kukosekana kwa viwanja maalumu vya mchezo huo ingawa
kuna mwamko wa jamii kushiriki na kuupenda mchezo huo huku akiishukuru Serikali chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuanza ujenzi wa viwanja mbalimbali na hamasa kubwa ya kuinua sekta ya michezo.
Ametoa wito kwa jamii na wahisani kusaidia kukuza mchezo huo wa Hockey hususan timu za majeshi Zanzibar kutoa wachezaji ambao watashiriki katika timu za wanawake za Hockey.
Kipa timu hiyo ya Royal Queens , Idaya Hassan, amesema mazoezi hayo ya pamoja yaliyofanyika katika viwanja vya JMK Youth Park, jijini Dar es Salaam, yamekuwa na ufanisi na yamesaidia wachezaji wa timu yake kujinoa kikamilifu.
Mratibu wa mchezo wa Hockey katika shule za Tanzania Bara , Elieza Mwankemwa, amesema mazoezi hayo ya wiki moja yameambatana na mafunzo mbalimbali kuiimnarisha timu hiyo ya wanawake kwani Zanzibar ilikuwa na timu nyingi za wanaume.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)




No comments:
Post a Comment