KAMPENI maalumu ya Darling Hair maarufu kama Loyalty Program, imezidi kushika kasi huku wasusi mbalimbali nchini wakiendelea kunufaika kwa njia mbalimbali wakati program hiyo ikiadhimisha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake.
Wasusi mbalimbali wakizungumza katika sherehe maalulu iliyofanyika Gongo la Mboto na kuwakusanya wasusi mbalimbali katika kuadhimisha miaka miliwi ya program hiyo, waliipongeza Darling Hair kwa kuwajali na kuwawezesha kiuchumi kwa kuwapa vifaa baada ya kujizolea pointi kutokana na kukusanya lebo za bidhaa za kampuni hiyo.
“Siku ya leo imekuwa muhimu sana kwetu kama wasusi kwa sababu tumekutana na kubadilishana mawazo, tumepata mafunzo na pia vifaa mbalimbali vya saluni kutoka Darling Hair. Kwa kweli hawa hawana mpinzani,” alisema Jackline Temba ambaye anamiliki saluni eneo la Kitunda Jijini Dar es Salaam.
Alitoa wito kwa wasusi ambao hawajajiunga na program hiyo ya loyalty kufanya hivyo ili nao wafaidike na wajinyanyue kiuchumi.
Naye Regina Filbert kutoka Kitunda alisema kupitia program hiyo wasusi wamejifunza mambo mengi kutokana na mafunzo ya mara kwa mara na pia wamejishindia zawadi nyingi katika miaka miwili ya kampeni hii.
“Binafsi kupitia kampeni hii nimeshinda viti, rollers na vifaa vingine baada ya kukusanya lebo hizi na kukusanya pointi zilizoniwezesha kushinda,” alisema.
Salumu Hamisi, maarufu kama DD kutoka eneo la Banana, alisema Darling Hair imekuwa familia kwa wasusi na imekuwa ikiwafuatilia kwa karibu mno ili kuhakikisha wanashugulikia changamoto zozote na wasusi wote wanafikiwa wakubwa kwa wadogo.
“Wamekuwa ni wasikivu sana na wanatufuatilia kwa karibu. Changamoto zetu nyingi tu wameshazishugulikia ndio maana bidhaa zao zinaendelea kuongoza sokoni,” aliongeza.
Alitoa wito kwa wasusi mbalimbali kuangalia vifaa wanavyohitaji na kujiunga na program hiyo ili washinde na kujiongezea mitaji ili wafanye boashara kwa wepesi.
Mwakilishi wa Darling Hair, Daniel Kisusange kutoka idara ya Masoko, alisema hafla hii iliwakutanisha wasusi kutoka Gongo la Mboto, Chanika, Pugu, Banana, Kitunda na maeneo mengine.
“Tulianzisha program hii ili turudishe kwa wateja wetu wakubwa ambao ni wasusi lakini pia tuliona umuhimu wa kuwakusanya wasusi wote pamoja ili wabadilishane mawazo na kupata ujuzi na maarifa mapya,” alisema.
Aliongeza kuwa hadi sasa wameshawafikia wasusi zaidi ya 10,000 na kufikia mwakani wanatarajia wasusi hawa wataongezeka maradufu. “Baada ya Dar es Salaam tutaelekea mikoani na tutapia Tanga, arusha, Morogoro, Dodoma, Iringa, Shinyanga na Geita,” alisema.






No comments:
Post a Comment