ALAF Limited kwa mara nyingine imeibuka mshindi katika Tuzo za Rais za mzalishaji Bora wa Mwaka (PMAYA), toleo la 19 hii ikiwa ni mara ya 17 mfulululizo tangu ianze kushiriki katika tuzo hizi..
Tuzo hii ya mshindi wa kwanza katika kipengele cha chuma na Bidhaa za chuma, ilikabidhiwa na Makamu wa Rais Mh. Deogratias Ndejembi.Tuzo hizi hutolewa na kuratibiwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI).
“Tuzo hii inadhihirisha uwajibikaji wetu katika kuzalisha katika viwango bora duniani, kuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi na kuwa sehemu ya ukuzaji wa viwanda Tanzania,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Hawa Bayumi.
Aliishukuru CTI, timu nzima ya ALAF na kila mteja anayeendelea kujenga pamoja na ALAF. “Asanteni kwa kutuunga mkono na imani yenu kwetu . Pamoja tutaendelea kujenga viwanda imara, jamii imara na Tanzania imara zaidi,” aliongeza.






No comments:
Post a Comment