JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Serikali Yaimarisha Usafiri Kurahisisha Wakulima Kufikisha Mazao Sokoni

Share This
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Gidius Kyaharara akipokea zawadi mfuko kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  Nicholas Kinyariri wakati  wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea  Banda la TASAC Maonesho ya Kilimo Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Dkt.John Samwel Malecela Nzuguni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SERIKALI imesema inaendelea kuimarisha miundombinu na huduma za usafirishaji ili kuwawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kwa usalama na kwa wakati, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa masoko na kupunguza hasara baada ya mavuno.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kyaharara, baada ya kutembelea mabanda ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Profesa Kyaharara amesema usafiri bora ni nguzo muhimu katika kuhakikisha mazao yanayozalishwa na wakulima yanafika sokoni kwa wakati na katika ubora unaotakiwa, hivyo kupunguza upotevu wa mazao na kuongeza kipato cha wazalishaji.

Amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira salama ya usafirishaji wa mazao kwa kuwa hatua hiyo inalinda juhudi na uwekezaji wa wakulima, huku ikihakikisha mazao yanafika katika maeneo yenye uhitaji bila vikwazo visivyo vya lazima.

Aidha, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa upatikanaji wa mitaji na uwekezaji katika sekta ya usafirishaji, hususan kipindi cha mavuno, ili kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda katika masoko mbalimbali nchini.

Profesa Kyaharara amesema Serikali pia inaendelea kuboresha miundombinu ya usafiri katika maeneo ya uzalishaji ili kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka mashambani hadi kwenye masoko ya ndani na nje ya maeneo ya uzalishaji.

Katika hatua nyingine, amesema Serikali inaendelea kuwaunganisha wakulima na masoko ya uhakika ili kuongeza thamani ya mazao yao, kuboresha kipato na kuwahamasisha kuongeza uzalishaji.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Gidius Kyaharara akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano wa   Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nicholas Kinyariri wakati Katbu Mkuu huyo alipotembelea Banda la TASAC Maonesho ya Kilimo Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Dkt.John Samwel Malecela Nzuguni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Gidius Kyaharara akisaini kitabu katika Banda Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati alipotembelea Banda la TASAC Maonesho ya Kilimo Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Dkt.John Samwel Malecela Nzuguni jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Gidius Kyaharara akiwa Katika picha ya pamoja na Watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  mara baada kupata kupata maelezo ya Shirika hilo wakati kweny Maonesho ya Kilimo Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Dkt.John Samwel Malecela Nzuguni jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad