JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NMB YAUNGA MKONO AFYA YA WATUMISHI KUPITIA SHIMISEMITA.

Share This

 Benki ya NMB imeendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuimarisha afya ya mwili na akili ya watumishi kupitia Mashindano ya Kitaifa ya SHIMISEMITA yanayoendelea mkoani Mbeya.

Mashindano hayo yanawakutanisha zaidi ya watumishi 5,000 kutoka halmashauri 184 nchini, huku NMB ikiendelea kuwa miongoni mwa wadau wanaoyaunga mkono.

Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Wogofya Mfalamagoha, alisema ushiriki wa benki hiyo unatokana na imani kwamba mtumishi mwenye afya ana nafasi kubwa ya kuwa na tija na kutoa huduma bora kwa wananchi. Katika mashindano ya mwaka huu, NMB imetoa Sh milioni 34.5 pamoja na jezi kwa timu zitakazofuzu hatua ya robo fainali katika mpira wa miguu, wavu, pete na kikapu.

Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, aliyemwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, aliipongeza NMB kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli zinazochangia ustawi wa watumishi na wananchi. Alisema michezo inasaidia kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi wa serikali za mitaa.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa, alisema ujio wa maelfu ya washiriki wa SHIMISEMITA pia umeongeza shughuli za kiuchumi mkoani humo. Kupitia mashindano hayo, michezo inaendelea kuwa jukwaa la kuimarisha afya na ushirikiano wa watumishi huku Tanzania ikijiandaa kuwa mwenyeji mwenza wa AFCON 2027 pamoja na Kenya na Uganda.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad