Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NIC Insurance imewahimiza wakulima nchini kutumia fursa ya Bima ya Kilimo ili kujikinga dhidi ya hasara zinazoweza kusababishwa na majanga mbalimbali ya asili na kulinda uwekezaji wao katika sekta ya kilimo.
Akizungumza katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela jijini Dodoma, Afisa Bima wa NIC Insurance, Aman Mollel, amesema bima hiyo inalenga kuwakinga wakulima dhidi ya madhara yanayosababishwa na ukame, mafuriko, magonjwa na wadudu wa mimea, pamoja na majanga mengine yanayoweza kuathiri uzalishaji na kipato.
Mollel amesema mazao yanayoweza kukatiwa bima ni pamoja na pamba, korosho, kahawa, tumbaku, maharage, mahindi, mpunga, shayiri, alizeti na chai.
Amesema bima hiyo pia inamlinda mkulima dhidi ya majanga kama vimbunga na mvua ya mawe, ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa mazao, kupunguza uzalishaji na kuathiri kipato cha mkulima.
Kwa mujibu wa Mollel, ili mkulima aweze kupata huduma hiyo anatakiwa kuwa na fomu ya maombi iliyojazwa na kusainiwa, taarifa za gharama za uzalishaji kwa hekta, makisio ya gharama au bei kwa kilogramu pamoja na taarifa za kihistoria za uzalishaji wa mkulima.
Amesema matumizi ya Bima ya Kilimo ni muhimu katika kuwawezesha wakulima kuendelea na shughuli zao za uzalishaji bila kukumbwa na athari kubwa za kifedha pale majanga yanapotokea.
“Bima ya Kilimo ni kinga ya mkulima dhidi ya majanga, hasara na changamoto zinazoweza kujitokeza katika uzalishaji wa mazao,” amesema Mollel.
Amesema NIC Insurance pia inatoa Bima ya Mifugo katika kumkinga mfugaji dhidi ya hasara inayoweza kujitokeza kutokana na vifo vya mifugo vitokanavyo na ajali ,Wizi wa Mifugo ,Magonjwa ,Uchinjwaji wa lazima kutokana na ushauri wa daktari.
Amesema Bima ya Mifugo iko katika mifugo ya Ng'ombe wa Maziwa ,Ng'ombe wa Nyama ,Kuku pamoja na Mbuzi katika vigezo kuwa na fomu ya maombi iliyosainiwa,ripoti ya ukaguzi wa mnyama kutoka kwa afisa mifugo pamoja na ratiba ya chanjo ya mifugo.
Mollel amesema gharama za Bima hizo kwa Ng'ombe wa Maziwa asilimia Tano kwa Makato ya ulinganifu wa asilimi a 10,Ng'ombe wa nyama asilimia Nne kwa Makato ya ulinganifu wa asilimi a 10,Kuku asilimia Tano kwa Makato ya ulinganifu wa asilimi a 15,Mbuzi asilimia Tano kwa Makato ya ulinganifu wa asilimi a 10
Amesema Ada ya Bima inapatikana kwa kuchukua kiwango cha asilimia kinachotolewa na Kampuni ya Bima kuzidisha na thamani ya mfugo au mnyama.
Ameongeza kuwa faida ya Bima ni kukuza uwekezaji ,kumrudisha mfigaji kwenye hali aliyokuwa nayo kabla ya mifigo kufa pamoja na kupata mkopo kutoka taasisi za kifedha kwa masharti nafuu.




No comments:
Post a Comment