MAONESHO ya uchumi bunifu yanayoenda kwa jina la Mashariki Creative Economy Expo 2026 yanaanza jijini Dar es Salaam kuanzia kesho tarehe 18 hadi 21 Agosti 2026, yakiwakutanisha wabunifu, wawekezaji, watangazaji, wamiliki wa haki, watunga sera na wabunifu wa teknolojia kwa ajili ya kukuza uchumi wa ubunifu barani Afrika.
Maonesho hayo yaliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Culture and Development East Africa (CDEA) yanalenga kuifanya sekta ya ubunifu kuwa chanzo cha fursa za biashara na uwekezaji, kupitia matumizi ya haki miliki (IP) katika muziki, filamu, fasihi, sanaa za picha, maudhui ya kidijitali na maeneo mengine.
Expo hiyo pia inalenga kujenga ushirikiano wa kimkakati na majukwaa ya habari na burudani kama Azam Max, ili kukuza simulizi za Afrika Mashariki, kuibua vipaji vipya na kuunganisha wabunifu na masoko mapana ya kikanda na kimataifa.
#MasharikiExpo2026 #UchumiWaUbunifu #CDEA #VipajiAfrika #HakiMiliki #DarEsSalaam #AfrikaMashariki

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


No comments:
Post a Comment