JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


IFM YAENDELEA KUTOA ELIMU INAYOENDANA NA MAHITAJI YA TEKNOLOJIA

Share This

 



Na Mwandishi Wetu, Dodoma
CHUO cha Uhasibu na Usimamizi wa Fedha (IFM) kimesema kimejipanga kuendelea kutoa elimu inayokwenda sambamba na mahitaji ya sasa ya teknolojia, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wahitimu wanakuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na uchumi wa kidijitali.

IFM imesema hayo wakati ikishiriki Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Ufugaji Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma ,Mwanza pamoja na Simiyu mbapo imeeleza kuwa ushiriki wake ni sehemu ya kusogeza huduma za elimu karibu na wananchi.

Kwa mujibu wa chuo hicho, ushiriki katika maonesho hayo ya kitaifa na ya kanda pia unalenga kuwafikia wananchi wanaozunguka kampasi zake na kuwapatia elimu pamoja na taarifa kuhusu fursa zinazopatikana kupitia programu mbalimbali za IFM.

IFM imeeleza kuwa maonesho hayo yamejikita katika kuongeza thamani ya mazao na bidhaa ili ziweze kupata masoko yenye tija, ambapo ujuzi wa usimamizi wa fedha ni muhimu katika kuhakikisha mnyororo mzima wa thamani unakuwa na tija kwa wazalishaji.

Chuo hicho kimesema pale mazao yanapoingia sokoni, masuala ya usimamizi wa fedha huwa muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata mapato yanayoendana na thamani ya uzalishaji wao, huku wakijengewa uwezo wa kutumia fedha hizo kwa ufanisi.

Aidha, IFM imeeleza kuwa elimu ya fedha na matumizi ya teknolojia ni muhimu kwa wakulima na wafanyabiashara katika kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za kifedha, kufanya maamuzi sahihi ya biashara na kuongeza tija katika shughuli zao za kiuchumi.












Matukio katika Picha Chuo cha  IFM  katika maonesho ya Kitaifa na Kanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad