Jumla ya washiriki 74, wakiwemo watoto 20, walishiriki katika zoezi hilo lililolenga kuchangia uhifadhi wa mazingira na kuhamasisha ushiriki wa wafanyakazi katika shughuli za maendeleo ya jamii.
Akizungumza kuhusu shughuli hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Kitengo cha Coverage wa Standard Chartered Bank Tanzania, Geofrey Mchangila, alisema:
"Zoezi la mwaka huu lina umuhimu wa pekee kwetu kwani linafanyika wakati Standard Chartered inaadhimisha miaka 20 ya kujitolea kwa jamii duniani kote. Tunaamini kuwa mabadiliko ya kweli huanza pale watu wanapounganisha nguvu zao.
Kupitia ushirikiano wetu na wafanyakazi, familia zao pamoja na Nipe Fagio, tunaendelea kuchangia kulinda ukanda wa pwani wa Tanzania na kujenga jamii zenye afya bora na mazingira endelevu kwa vizazi vijavyo."
Katika zoezi hilo, washiriki walisafisha eneo lenye ukubwa wa takribani mita za mraba 4,000 za ufukwe na kukusanya kilo 506 za taka zilizohifadhiwa katika mifuko 55.

Uchambuzi wa taka zilizokusanywa ulionyesha kuwa plastiki, hususan povu la polystyrene na chupa za plastiki za vinywaji, ndizo zilikuwa taka zilizopatikana kwa wingi, hali inayodhihirisha umuhimu wa kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti uchafuzi wa mazingira ya bahari.
Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kupitia ushirikiano wake na Nipe Fagio, Standard Chartered Tanzania imefanikisha jumla ya kampeni tano za usafi wa fukwe, ikihusisha washiriki 594, kusafisha zaidi ya mita za mraba 32,000 za ukanda wa pwani na kukusanya karibu tani tano za taka.
Mpango huu ni sehemu ya mkakati mpana wa Standard Chartered wa kuendeleza uhimilivu wa mazingira na maendeleo endelevu, huku ukiunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), hususan Lengo la 13 la Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, Lengo la 14 la Kuhifadhi Maisha ya Chini ya Maji na Lengo la 17 la Kuimarisha Ushirikiano kwa Ajili ya Kufanikisha Malengo.
Standard Chartered inapoendelea kuadhimisha miaka 20 ya programu yake ya kujitolea kwa jamii, inaendelea kuwahamasisha wafanyakazi wake kutumia muda, ujuzi na utaalamu wao kuleta mabadiliko chanya na endelevu katika jamii na mazingira.

No comments:
Post a Comment