JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUBADILI MTINDO WA KAZI ILI KUFIKIA DIRA 2050*

Share This

 


SERIKALI imesema hakuna tena biashara ya kawaida kwa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali. Waziri Prof. Kitila Mkumbo amesema viongozi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia matokeo, ubunifu na uwajibikaji ili kuharakisha Dira ya Taifa 2050.

Akizungumza Kibaha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi 57, Prof. Mkumbo amesema lengo la Taifa ni kufikia uchumi wa dola Trilioni 1 ifikapo 2050. Amesema hilo litafanikiwa kama viongozi watatafsiri maono hayo kuwa huduma na miradi inayoonekana kwa wananchi.

Waziri amesisitiza kuwa mafanikio hayatapimwa kwa vikao bali kwa tija, uwekezaji na ajira. Pia amewataka viongozi kushirikiana na sekta binafsi kwani ndio injini ya ukuaji wa uchumi. "Tuache kuwa vikwazo kwa wawekezaji" amesema.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu amesema tangu 2024 viongozi 187 wameshafundishwa. Matokeo yake makusanyo ya gawio yameongezeka kutoka Sh bilioni 637 hadi Sh Trilioni 1.3. Ofisi yake imeweka vipaumbele 5 vya mageuzi ikiwemo utawala bora na ubia wa umma na binafsi

Katika mafunzo ya siku 4, viongozi watapata mafunzo ya uongozi wa kimkakati, usimamizi wa uwekezaji na utawala bora.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad