Na Mwandishi Wetu
OFISI ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema kwa mujibu wa sheria ya Maadili ya 1995 inatoa ruhusa kwa mwananchi au mtu yeyote kuona mali ya kiongozi wake.
Hayo ameyasema Afisa Maadili, Grace Matunda, akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotaka kufahamu uwazi wa mali za viongozi wakati walipotembelea Banda la Maadili kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba).
Amesema mwananchi ataona mali ya kiongozi wake kwa kufuata utaratibu wa Sheria kwa kulipia ada ya shilingi 1000 kwa kuandika Barua kwa Kamishna wa Maadili akianisha majina ya kiongozi na kutoa sababu ni kwanini anataka kukagua au kuona mali ya kiongozi.
“Isipokuwa mwananchi hatakiwi kurekodi, kupiga picha au kwenda kutangaza kwa umma au kwa mtu yeyote, kwani sababu ya kuweka hivyo ni kutunza utu na usiri wa kiongozi wa Umma kama ilivyo kwa wananchi wengine ambao hawataki mali zao ziwe wazi” amesema Grace.
.jpeg)


No comments:
Post a Comment