JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Rais wa Zanzibar Ajumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa , Ashiriki Sala ya Jeneza ya Marehemu Sheikh Abdullah Hamid Suleiman

Share This

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Baada ya Sala ya Ijumaa, Rais Dkt. Mwinyi ameshiriki Sala ya Jeneza ya Marehemu Sheikh Abdullah Hamid Suleiman, aliyekuwa Khatibu katika misikiti mbalimbali Zanzibar, iliyosaliwa katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar.

Marehemu Sheikh Abdullah Hamid Suleiman, amefariki dunia leo, tarehe 31 Julai 2026, na kuzikwa kijijini kwao, Muungoni, Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad