Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na Benki ya CRDB katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 14 Julai 2026, alipokutana na uongozi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, waliofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo.
Amesema Serikali inathamini mchango wa benki hiyo katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo na itaendelea kufanya kazi kwa karibu katika ujenzi wa skuli, nyumba za makaazi, miradi ya kilimo na kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wananchi.
Aidha, ameipongeza CRDB kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya umma na kuisaidia Serikali kupata mikopo kutoka taasisi za fedha za kimataifa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Prof. Neema Munisi Mori, amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na programu za kuwawezesha vijana, wanawake na wajasiriamali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela, ameipongeza Serikali kwa maendeleo yaliyofikiwa na kuanzishwa kwa akaunti maalum ya kulipa madeni ya mikopo ya miradi ya kimkakati, hatua iliyoongeza ufanisi na kuimarisha imani ya taasisi za fedha kwa Serikali.



.jpeg)


.jpeg)


.jpeg)



.jpeg)


No comments:
Post a Comment