JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NMB Yawezesha Wakulima Kumiliki Matrekta kwa Malipo ya Awamu

Share This
Benki ya NMB imeongeza nguvu katika sekta ya kilimo kwa kutoa suluhisho za kifedha zinazowawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao kupata mitaji, kununua mazao, kuyachakata na kuyapeleka katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika Banda la NMB kwenye Maonesho ya SabaSaba, Mkuu wa Idara ya Kilimo kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalugenge, alisema huduma hizo zinawalenga wadau waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo, hasa katika msimu wa mavuno ya mazao kama kahawa, tumbaku, ufuta na pamba.

NMB pia imeendelea kuwawezesha wakulima kumiliki matrekta na mashine nyingine za kilimo kwa utaratibu wa malipo ya awamu. Meneja Mahusiano Kitengo cha Kilimo kutoka Makao Makuu ya NMB, Elias Leasa, alisema mkulima anaweza kuanza kwa kulipa asilimia 10 ya thamani ya kifaa na kuendelea kulipa kulingana na msimu wa mavuno.

Mnufaika wa mpango huo, Dustan Alan Bembati, alisema kupata trekta kutapunguza changamoto ya kusubiri huduma ya kulima kwa muda mrefu kutokana na uhaba wa matrekta ya kukodi. Alisema mpango huo unaweza kusaidia wakulima kuongeza tija, kupunguza gharama na kuimarisha uzalishaji.

Meneja Mahusiano Kitengo cha Kilimo kutoka Makao Makuu ya Benki ya NMB, Elias Leasa, akikabidhi funguo za trekta kwa Dustan Alan Bembati, mnufaika wa mpango wa ufadhili wa vifaa vya kilimo wa NMB, wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Maonesho ya SabaSaba jijini Dar es Salaam.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad