JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NIC Insurance Yatoa Elimu Kuhusu Bima ya COMESA kwa Wamiliki wa Vyombo vya Moto

Share This

 



Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya NIC Insurance imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Bima ya COMESA (COMESA Yellow Card), ikieleza kuwa huduma hiyo inarahisisha safari za kuvuka mipaka ya nchi wanachama wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) bila kulazimika kukata bima mpya ya lazima katika kila nchi.

Akizungumza katika Banda la NIC Insurance kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Afisa Mwandamizi wa kampuni hiyo, Bi. Erika Nnko, amesema Bima ya COMESA ni mfumo wa kikanda wa bima ya vyombo vya moto unaowapa madereva uhuru wa kusafiri kwa usalama katika nchi wanachama wa COMESA huku wakitambuliwa kisheria kupitia kadi maalumu ya njano inayofahamika kama COMESA Yellow Card.

Amesema mmiliki wa chombo cha moto anapokata bima hiyo kupitia kampuni za bima zilizoidhinishwa nchini, hupatiwa Yellow Card ambayo hutambulika na mamlaka za nchi zote zinazoshiriki katika mfumo huo.

Erika amesema kadi hiyo hutoa kinga dhidi ya madai yanayotokana na majeraha kwa watu wengine au uharibifu wa mali za watu wengine unaoweza kusababishwa na chombo cha moto wakati wa safari katika nchi wanachama wa COMESA.

Ameeleza kuwa mfumo huo unarahisisha biashara na usafirishaji wa mizigo pamoja na safari za watu binafsi kwa kuondoa ulazima wa kukata bima mpya ya lazima ya mkataba wa tatu (Third Party) kila unapovuka mpaka wa nchi mwanachama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad