JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WALES, GHANA KUPIMANA NGUVU KABLA YA MASHINDANO MAKUBWA

Share This

 


TIMU ya Taifa ya Wales itashuka dimbani leo Juni 2 kuikaribisha Ghana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa saa 21:45 usiku kwenye Uwanja wa Cardiff City nchini Uingereza.

Mchezo huu unatajwa kuwa wa kihistoria kwani ni mara ya kwanza kwa Wales kucheza dhidi ya taifa la Afrika katika mchezo wa kimataifa wa wanaume, huku pia ukiwa mkutano wa kwanza kabisa kati ya mataifa haya mawili.

Wales chini ya kocha Craig Bellamy itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kuendelea kujenga kikosi chake kuelekea michuano ijayo ya UEFA Nations League. Bellamy amekuwa akisisitiza soka la kushambulia kwa kasi, presha kubwa kwa wapinzani na matumizi ya wachezaji wa pembeni, jambo ambalo linaweza kuipa Wales faida ya kucheza mbele ya mashabiki wake wa Cardiff.

Kwa upande wa Ghana, Black Stars wanautumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2026. Kikosi hicho kinachonolewa na Carlos Queiroz kimewasili Wales na baadhi ya nyota wake wakubwa akiwemo Antoine Semenyo, Jordan Ayew, Thomas Partey pamoja na Iñaki Williams. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Mohammed Kudus kutokana na majeraha kunaweza kupunguza ubunifu wao katika eneo la ushambuliaji.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kiufundi, mchezo huu unaweza kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na tofauti za mitindo ya timu hizo. Wales wanapendelea kumiliki mpira na kufanya mashambulizi ya haraka kutoka pembeni, wakati Ghana hutegemea nguvu, kasi na mipira ya kushtukiza kupitia washambuliaji wake. Vita kubwa vinatarajiwa katikati ya uwanja ambapo Thomas Partey atakuwa na jukumu la kuzuia kasi ya viungo wa Wales.

Kwa ubora wa vikosi na maandalizi ya sasa, mchezo huu unaonekana kuwa wazi kwa timu zote mbili. Wales wana faida ya uwanja wa nyumbani na sapoti ya mashabiki wao, lakini Ghana wana wachezaji wengi wanaocheza ligi kubwa za Ulaya wenye uwezo wa kubadilisha matokeo wakati wowote. Jisajili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad