Na Mwandishi Wetu
WADAU wa Maendeleo kutoka Kata ya Kisaka Wilayani Serengiti mkoani Mara wamefungua Kesi dhidi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzani (JWTZ), Kikosi 27 KJ Makoko, kukalia kimabavu Vijij vitatu vya Borenga, Buchanchali na Marembota.
Kwa mujibu ya barua ya wito kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kulitaka Jeshi hilo kupitia Kikosi cha 27KJ Makoko Tarehe 29 Julai mwaka huu kulitaka kwenda Mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikiliza shauri hilo.
Kwa mujibu ya malamiko ya wakazi wa kata hiyo hapo awali tayari walishaandika barua mpaka kwa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dk. Samia Saluhu Hassan, kuomba kuingilia kati mgogoro huo kati ya Kikosi 27kj na wakazi hao uliodumu tokea mwaka 2016 mpaka hivi sasa
Aidha, katika barua hiyo wakazi hao tayari wameliomba jeshi hilo kuwa mwaka 2008 waliingia katika eneo hilo linalolalamikiwa na kuanza kufanya mazoezi ya kijeshi, kwa makubaliano ya kupewa Hekali 40 za Kijiji cha Nyiboko tu na siyo kwa Vijiji vingine.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka Wizara ya Ardhi na nakala ya barua inaonyesha kuwa wizara hiyo, imekiri (JWTZ), kuwa eneo ambalo wamepewa ni katika Kijiji cha Nyiboko tu siyo vijiji vingine inavyovikalia kimabavu.
Imeelezwa kuwa, kitendo cha kuendelea kukalia kimabavu vijiji vingine kwa kikosi hicho na kuwazuia wananchi kufanya shughuli zao za Kilimo, Ufugaji, Uchimbaji wa Mawe (Vigae), Madini, njia za kupita watu na shughuli za Kimila (Matambiko) ni ukiukwaji ni ukiukwaji wa misingi ya haki za binadamu na Utawala Bora.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka katika Kikosi hicho na zilizosambaa zaidi kutoka katika kata hiyo, zinadai kuwa Jeshi hilo limetoa onyo kali tabia ya baadhi ya wanachi kuvamia maeneo hayo na kufanya shughuli zao za kijamii katika vijiji vya Nyiboko Borenga na Marembota.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba inaomba kuwa wananchi waelimishwe kuacha kufanya shughuli za kijamii katika eneo hilo na kuendelea kusema kuwa kwa yoyote atakae kiuka na kuendelea kufanya shughuli hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake.
Aidha, kwa wale waliojenga nyumba katika vijiji hivyo wajulishwe na kuziondoa wenyewe na kutafuta maeneo mengine kabla ya tarehe 14 ya mwezi wa 7 mwaka huu.
Mmoja wa mdau ambaye hakutaka jina lake liandikwe amesema kuwa iweje jeshi la wanachi JWTZ kikosi 27kj makoko watoe taarifa kuwa wananchi waelimishwe na kuhama katika maeneo hayo wakati wanajua kuwa kuna Kesi ya msingi imefunguliwa na tayari tarehe ya kuanza kusikiliza shauri imepangwa.
Mdau huyo alieleza kuwa kumeanza utaratibu mpya kwa wakazi katika kata hiyo ya kisaka kuandika barua na kuomba kutoka katika Kikosi hicho cha (JWTZ) kibali cha kufanya shughuli za kijamii katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa mdau huyo ameeleza kuwa kitendo kinachofanywa na Kikosi hicho ni unyanyasaji na ukiukwaji wa Haki za Binadamu na tunaomba Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama atusaidie wakina mama ambao wanapata tabu ya kukata kuni za kupikia, fito za kuwezeka Nyumba na kuchota maji ya matumizi ya Nyumbani.
"Tunanyanyasika sana hakuna sehemu ya kilimo sehemu hiyo ilitengwa kwa ajili ya kilimo, malisho na matambiko tunaomba serikali ya (CCM), ikiongozwa na Rais Dk, Samia atusikie kilio chetu, "
Mkazi mwingine ambaye naye hakutaka kutajwa jina lake, alisema kuwa Kwa ujumla hali ni mbaya katika maeneo hayo, kwani maeneo yalitolewa na kitongoji cha Misheni lakini vitongoji vya Center na Mtakuja, havikushirikishwa wala tangazo la mkutano wa kijiji halikuwepo na huo si utaratibu mzee huyo mstaafu alilamimika,
Kwa mujibu wa Mzee huyo, alilalamika kuwa Kama kweli (JWTZ) hawa ni walinzi kwanini wajiushishe na kwenda kuweka kambi kwenye machimbo wasiende kule katika Kijiji cha Masaba Porini iweje washikilia katika vijiji hivyo ambavyo kuna machimbo ya udongo wa Madini.
Mzee huyo aliendelea kusema kuwa hapo, kuna siri Leo vijiji havipati gawio wala vijana wetu wamefukuzwa na pale ni biashara tu na mbaya zaidi kiwanda kimejengwa kata ya jirani na mali inatoka Kata ya kisaka na kwenda kuwafaidisha watu wengine huku vijana wetu wakikosa ajira.
Mzee huyo alimalizia kusema kuwa wanamuomba Mkuu wa Majeshi na Waziri wa Ulinzi kufuta hii kambi na sisi wananchi tupo tayari kutoa eneo lingine la kambi na kuja kuchukua maeneo yetu ambayo ndio tengemeo letu .
Alisema kuwa, wanalipenda Jeshi lao hata wazee wao robo ya kijiji walikuwa ni wanajeshi, je! hawakuliona eneo hili hata Kanali wa kwanza waTanzania anatoka katika Kata ta Kisaka col William Makori Chacha na maofisa wingine wengi bado wapo kazini.
Na kumalizia kwa kusema kuwa hawana sehemu ya ziada ya kilimo na eneo hilo lilitolewa mwaka 1974 kwa ajili ya vijiji vya ujamaa.


No comments:
Post a Comment