JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NMB yafungua tawi Mvuha, yakata safari ya kilomita 8

Share This

WAKAZI wa kata ya Mvuha na maeneo jirani wameondokana na safari za hadi kilomita 80 kufuata huduma za benki Morogoro mjini, baada ya kuzinduliwa kwa Tawi la NMB Mvuha ambalo sasa limesogeza huduma za kifedha karibu na wananchi.

Tawi hilo, lililojengwa kwa gharama ya Sh milioni 296, linakuwa la 251 katika mtandao wa NMB unaohudumia zaidi ya wateja milioni 10 nchini. Linawahudumia wananchi, wakulima, wafanyabiashara, Serikali na taasisi mbalimbali.

Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango, alisema tawi hilo pia litatoa elimu kuhusu kupanga matumizi, kuweka akiba, kukopa kwa tija na kutumia huduma za kifedha kwa usalama.

Uzinduzi huo uliongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, ambaye aliipongeza NMB kwa kuendelea kusogeza huduma za kifedha mijini na vijijini."Endeleeni kuwafikia na kuwahudumia Watanzania popote walipo,”alisema Bw.Michael.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad