JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NACTVET Yaratibu Shindano la Ububevu wa Ushonaji Kujiandaa Mashindano ya Kidunia

Share This

Mdhibiti Ubora Mkuu wa NACTVET Nicholaus Moshi akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na Shindano la Ubunifu wa Ushonaji wa Mavazi kwa Kanda ya Dar es Salaam lililofanyika Chuo cha Anna Academy.Mkurugenzi wa Chuo cha Anna Academy Anna Lunguya akizungumza kuhusiana mashindano hayo katika ubunifu wakiwa ndio watarajiwa wa kuiwakilisha nchi kudunia katika mashindano baada ya kufanyika mchujo wa kitaifa.

Washiriki Tisa wakijiandaa katika shindano la ubunifu wa Ushonaji wa  mavazi.

Picha katika Makundi mbalimbali wakati wa maandalizi ya Shindano la Ubunifu wa Ushonaji Mavazi lililofanyika katika Chuo cha Anna Academy.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
NCHI  ya Tanzania kushiriki mashindano ya ubunifu na ubobezi wa katika Fani Tisa kwa kushirikisha wanafunzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi ambapo washindi wataopatikana katika Kanda wataingia ngazi Kitaifa watachunjwa kujiandaa kuwakilisha nchi kidunia.

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa NACTVET Joffrey Oleke amesema mashindano yalianza katika ngazi ya vyuo ambao washindi wanaingia katika mashindano ya kikanda.

Mashindano katika Fani ya ubunifu wa Ushonaji wa Mavazi Kanda ya Dar es Salaam yamefanyika katika Chuo cha Anna Academy kwa washiriki Tisa katika fani hiyo ambapo Katika mchujo watabaki wa tano ambao wataingia katika mashindano ya Kitaifa yatayofanyika mkoani Tanga Agasti Mwaka huu.

Akizungumza kwenye Mashindano Ubunifu wa Ushonaji wa Mavazi Mdhibiti Ubora Mkuu wa NACTVET Kanda ya Mashariki, Nicholaus Moshi, amesema mashindano hayo ni jukwaa muhimu la kuibua vipaji, kukuza ubunifu na kuandaa vijana watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya ngazi za kikanda na kimataifa.

Washiriki Tisa wanatoka maeneo mbalimbali ambao wanapimwa uwezo wao katika ubunifu, ukataji na ushonaji wa mavazi kwa kutumia viwango vya kimataifa.

Amesema washiriki hao wanatarajiwa kuchujwa ili kupata washindi watakaowakilisha Tanzania katika hatua zinazofuata za mashindano ya ujuzi ngazi ya kikanda na kimataifa.

“Mashindano haya yanalenga kupima uwezo wa vijana wetu katika ubunifu, ushonaji na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika sekta ya mavazi. Tunafurahi kuona vijana wameandaliwa vizuri kisaikolojia, kitaaluma na kwa vitendo ili kuonyesha uwezo wao,” amesema Moshi.

Ameongeza kuwa vifaa vinavyotumika katika mashindano hayo ni vya kisasa na vinavyotumika katika tasnia ya ubunifu na ushonaji duniani kote, jambo linalowawezesha washiriki kupata uzoefu unaokidhi viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ana Collection Academy, Anna Lunguya, amesema taasisi hiyo inajivunia kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambayo yana mchango mkubwa katika kukuza sekta ya ubunifu na ushonaji nchini.

Amesema sekta ya ubunifu na ushonaji imekuwa chanzo muhimu cha ajira na biashara kwa vijana wengi, hivyo mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji vipya na kupata wabunifu watakaoweza kuiwakilisha Tanzania katika ngazi mbalimbali za Afrika na duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad