MCHEZO wa Canada dhidi ya Qatar unatarajiwa kuwa mmoja wa mechi zenye ushindani mkubwa katika Kundi B la michuano ya Dunia 2026, ukipigwa usiku wa kuamkia Juni 19 saa 01:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Timu zote zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa na pointi moja baada ya kutoka sare katika mechi zao za kwanza, jambo linalofanya pambano hili kuwa muhimu sana katika mbio za kufuzu hatua ya mtoano.
Canada itaingia ikiwa na faida ya kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wake mjini Vancouver. Kikosi cha kocha Jesse Marsch kilionyesha uwezo mkubwa wa kushambulia katika sare ya 1-1 dhidi ya Bosnia na Herzegovina, huku mshambuliaji Jonathan David akiendelea kuwa tegemeo lao kubwa mbele. Hata hivyo, suala la utimamu wa nahodha Alphonso Davies linaendelea kufuatiliwa baada ya kuwa na majeraha yaliyomfanya akose sehemu ya maandalizi ya awali ya mashindano.
Kwa upande wa Qatar, walionyesha uthabiti mkubwa walipolazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Switzerland, timu iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda. Kikosi hicho chini ya kocha Julen Lopetegui kinategemea ubunifu wa Akram Afif na uzoefu wa Almoez Ali katika safu ya ushambuliaji. Qatar imeonyesha uwezo wa kucheza kwa nidhamu ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza, jambo ambalo linaweza kuwasumbua wenyeji ikiwa watapata nafasi za mashambulizi ya haraka.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi
Kiuchezaji, Canada huonekana kuwa na kasi kubwa zaidi, nguvu za kimwili na uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za mabao. Qatar kwa upande mwingine imejikita zaidi katika mpira wa kusubiri na kutumia makosa ya wapinzani. Kutokana na mazingira ya nyumbani na ubora wa wachezaji wake wa kushambulia, Canada inaweza kutawala umiliki wa mpira kwa muda mwingi wa mchezo huku Qatar ikisaka nafasi za kushtukiza.



No comments:
Post a Comment