JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Waziri Mkuu Aipongeza NEMC Kwa Miaka 40

Share This



*Aahidi Kusimama Kidete Iwe Mamlaka

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba amezindua mfumo mpya wa kidijitali wa kufuatilia uchafuzi wa mazingira wa Baraza la Taifa la Hufadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Amefanya uzinduzi huo leo Mei 28,2019 jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa baraza hilo mwaka 1986.

Maadhimisho hayo ambayo yaliambatana na maonesho ya masuala ya mazingira yamewashirikisha wageni mbalimbali wa serikali na wadau wa sekta binafsi wanaojihusisha na uhifadhi wa mazingira.

Dkt Mwigulu alianza kwa kuipongeza NEMC kwa kazi kubwa ambayo wameifanya kwa miaka yake 40 ya kuhifadhi mazingira akisisitiza kuwa bila mazingira safi binadamu na viumbe wengine wako hatarini kutoweka.

Amesema kazi ya kupambana na waharibifu wa mazingira siyo nyepesi na ndiyo sababu yeye binafsi atasimama kidete kuhakikisha NEMC inakuwa mamlaka ili ipate nguvu ya kukabiliana na wahalibifu wa mazingira.

Aidha, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamazingira namba moja hali ambayo ilifanya atunukiwe tuzo kama kinara wa mazingira duniani kwa kupigia chapuo uhifadhi wa mazingira nchini.

“Mwanamazingira namba moja Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amenituma niseme hapa kwamba anatambua mchango wenu na ataendelea kushirikiana nasisi wote kwenye ulinzi wa mazingira, mheshimiwa Rais amekuwa mstari wa mbele kutunza mazingira na ameahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele,” amesema Dkt Mwigulu

Amesema ingawa kuna watu wanalichukulia kwa wepesi suala la mazingira lakini tumeanza kuona athari za uhalibifu wa mazingira dhahiri kwenye maeneo mbalimbali nchini.

“Hapo zamani tuliona kama hadithi tu lakini sasa madhara ya kutojali mazingira yameanza kuja kwetu. Hili jambo siyo nadharia na si la kulichukulia kimzaha mzaha hata kidogo na shughuli za binadamu zimeongezeka kwa kasi mno hali ambayo inahatarisha mazingira,” alisema

“Watu wanaamua tu kukata miti ambayo wala wakati mwingine hawana haja nayo baada ya hapo. Mnakata miti mnasababisha jangwa tunakosa maji, mvua hakuna na ushindani wa matumizi ya ardhi unaongezeka kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi na za binadamu kwa hiyo lazima tukubali kubadilika hatuwezi kwenda na mtindo ule ule wa maisha,” amesema Waziri Mkuu na kuongeza

“Tusipokubali kubadilika tutalazimishwa na yatakayotokea baadae na kwa kuwa NEMC inatakiwa kuwa mamlaka mimi nitasimama kidete iwe mamlaka, mchakato wake utapita Baraza la kazi sasa huko mimi ndiye Mweyekiti nawaaahidi nitalisimamia NEMC iwe mamlaka,”

Aidha, Dkt Mwigulu amesema Rais Samia ameongeza bajeti ya kilimo zaidi ya mara 5 kuwezesha kilimo cha umwagiliaji ili kuondoa mazoea ya wakulima kufyeka mapori na kuharibu mazingira wanapoongeza mashamba.

“NEMC inahitaji kuongezewa meno ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mazingira na miaka 30 ijayo inakadiriwa kuwa watanzania tutafika milioni 100 na zaidi kwa hiyo lazima NEMC iwe na nguvu kukabiliana na ongezeko la shughuli za binadamu zinazohalibu mazingira,” amesema

“Pamoja na mafanikio tuliyoyapata bado kuna kazi kubwa kufanya mambo makubwa kwenye miaka 40 ijayo. NEMC endeleeeni kutoa elimu ya mazingira kuanzia ngazi ya familia watu wajue umuhimu wa kutunza mazingira,” amesema



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad