Uongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Karimu Meshack umewasili jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano mkuu wa Mwaka wa TAGCO unaotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza kuanzia tarehe 1-5 Juni, 2026..jpeg)
.jpeg)
Ukiwa Jijini Mwanza uongozi huo umemtembelea mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda kwa lengo la kujitambulisha na kumuelezea ratiba ya mkutano huo ambapo maafisa Mwasiliano wa Serikali watapata wasaa wa kubadilishana uzoefu, mbinu mbalimbali za kuimarisha utendaji kazi, mafunzo, kuhamasisha shughuli za kijamii, kushiriki michezo na kuhamasisha utalii wa ndani ambapo zaidi ya wanachama 500 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

.jpeg)



No comments:
Post a Comment