JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RC RUVUMA ATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUPOKEA ELIMU YA KODI NA KUELEZA CHANGAMOTO ZAO

Share This

 


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Ahmed Abbas amewataka wafanyabiashara wa Ruvuma kuwapa ushirikianao waafisa wa TRA watakaopita katika maduka yao ili kuweza kuwapatia elimu ya kodi sambamba na kueleza changamoto zao ili ziweze kutatuliwa.

Ameyasema hayo alipokutana na maafisa wa TRA waliofika ofisi kwake kwa lengo la kumjulisha juu ya uwepo za zoezi la Elimu ya kodi ya mlango kwa mlango wakiongozwa na meneja wa mkoa huo Nicodemas Mwakileme.

Aidha, amewaasa wananchi wa Ruvuma kutojihusisha na biashara ya magendo akisema vitendo hivyo vinaokesesha serikali mapato ambayo yangetumika kujenga vituo vya afya, barabara na mambo mengine kwa maendeleo ya nchi.

Kwa Upande wake, kiongozi wa timu hiyo ya zoezi la Elimu ya kodi mlango kwa mlango Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Salim Bakari amesema zoezi hilo litaendeshwa kwa wiki mbili katika Wilaya ya Songea, Nyasa, Mbinga na Tunduru yenye lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya mambo mbalimbali ya kodi na kuwahamasisha wananchi wa mipakani kutojihusisha na magendo kwa kuwaelezea athari za magendo na njia sahihi za kuingiza na kutoa bidhaa nchini.

Naye, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Ruvuma, Alhaji Issa Mzee ameipongeza TRA kwa kuja na zoezi hilo kwani litawasaidia wafanyabiashara kueleza changamoto zao ili kuweza kutatuliwa huku akiwasihi kutoa ushirikiano kwa maafisa hao kulipa kodi kwa wakati ili kuweza kujenga vituo vya afya barabara na mambo mengine ya maendeleo.

Mmoja wa wafanyabiashara waliotembelewa na maafisa hao, Olita amesema ameifaidika na elimu hiyo na amejifunza umuhimu wa kutumia mashine za EFD ili kuwa kupata rikodi sahihi za mauzo yao na kusadia kuweza kupata makadirio sahihi ya biashara zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad