*Awataka wananchi kuzitazama vyema fursa zitakazotokana na mashindano hayo kujikwamua kiuchumi
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa viwanja vya farasi na leaders club wilayani kinondoni ambavyo ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya mazoezi wakati wa mashindano ya AFCON na kumtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi kwa wakati ambapo ameitaka Halmashauri kuyatumia mashindano hayo kibiashara kwa kuhamasisha utalii lakini pia kutengeneza mazingira wezeshi kwa wananchi kufanya biashara mbalimbali ili kujiongezea kipato
Akizungumza akiwa katika muendelezo wa ziara zake katika Mkoa huo kwenye viwanja vya farasi Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam RC Chalamila ameitaka Halmashairi hiyo kufanya maboresho ya fukwe zake ikiwemo Coco beach ili ziweze kutumika vyema kuhamasisha utalii wakati wa AFCON huku akishauri kuwepo kwa utalii wa vyakula mbalimbali vya kitanzania hivyo ameitaka Halmashauri kuweka mazingira bora kwa watanzania kufanya biashara ikiwemo ya vyakula
Aidha RC Chalamila ameweeka msisitizo kwenye kukamilika kwa viwanja hivyo kwa wakati ili kumpa heshima Rais Dokta Samia ambae amepata heshima kubwa ya kimataifa ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya AFCON
Akiwa katika viwanja vya Leaders RC Chalamila ameelekeza kuimarisha kwa miundombinu ya barabara, upatikanaji wa huduma bora za maji safi na salama lakini pia kuimarishwa kwa mifumo ya ulinzi na usalama ikiwsmo kuwepo kwa taa za barabarani na ametumia nafasi hiyo kuhamasisha usafi na utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amewahakikishia wananchi kuwa uboreshaji wa viwanja hivyo vya farasi na Leaders Club hautaathiri matumizi ya wananchi ya viwanja hivyo hususani kwa matukio mbalimbali ya kijamii pamoja na mbio za mwendapole ambazo zimekuwa na mchango mkubwa wa kusaidia kukabiliana na magonjwa yasio ya kuambukiza ikiwemo shinikizo la damu na kisukari.
.jpeg)






No comments:
Post a Comment