Chato, Mei 29, 2026 – Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ameshiriki katika ibada na shughuli za mazishi ya mama mzazi wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Mazishi hayo yamefanyika leo Wilayani Chato, Mkoa wa Geita.
Marehemu Suzana Magufuli alifariki dunia jioni ya Jumatatu, Mei 25, 2026 nyumbani kwake Wilayani Chato, Mkoa wa Geita.
Mazishi hayo yameongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi. Yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Kassim Majaliwa, pamoja na viongozi wa kisiasa, kidini na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.







.jpeg)




No comments:
Post a Comment