JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ULINZI WA AJIRA NI GHARAMA KWA MLIPA KODI? ULINGANISHO WA TANZANIA NA BOTSWANA - KUELEKEA MEI MOSI

Share This

 


Na David KAFULILA, Aprili29,2026
JANA PPP CENTRE tulikuwa na kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi. Pamoja na kuwapongeza kwa mafanikio makubwa ya kufanya Agenda ya PPP kueleweka kwa kasi kwa umma na mfumo mzima wa Serikali kiasi Dira na Mpango wa muda mrefu( LTPP) na Mpango wa Nne wa miaka5( FYDPIV) kuonesha PPP kuwa nguzo muhimu kwa ufanikishaji, zaidi ni mafanikio bayana kwamba wakati awamu ya sita inaanza , miradi ya PPP ilikuwa ya thamani ya 1bn Dollar- 2.5Trilioni( Financing Strategy 2021/22 - 2025/26. ), ndani ya miaka4, thamani ya miradi ya Ubia imeongezeka kwa 8.5Trilion.

Hata hivyo niliwapa changamoto moja kuhusu namna Sheria ya Utumishi wa Umma inavyomlinda Mtumishi kwa gharama ya mlipa kodi. Niliwaeleza kuwa sheria iliwekwa kumlinda mtumishi dhidi ya matumizi mabaya ya viongozi wabaya ingawa sasa inaonekana kuwa mwiba kwa mlipa kodi kwani ugumu wa kumwondoa mtumishi asiyefaa ni mzigo kwa kumlipa kodi.

Niliwapa mfano wa nchi kama Botswana, wao mtumishi akiwa na utendaji mbovu kwa miaka miwili mfululizo anafukuzwa mara moja na endapo atakata rufaa , anakuwa nje ya Utumishi. wakati Tanzania utumishi unakoma baada ya rufaa zote kuamuliwa.

Mtumishi akifukuzwa Tanzania inachukua mpaka miezi22 kufukuzwa rasmi wakati Botswana hatua zote ni miezi3.

Kwa Mujibu wa Ripoti ya CAG ya Machi2024, inaonesha kwamba kati ya wafanyakazi 1124 waliothibitika kuwa na utendaji hafifu kwa miaka2 mfululizo katika kipindi cha mwaka 2022/23, Ni watendaji 138 tu waliofukuzwa sawa na asilimia 12%( mfumo wa rufaa unawapa ushindi).

Wakati Botswana kwa kipindi hicho 2022/23 , kati ya wafanyazi 241 waliothibitika kuwa na utendaji mbovu kwa miaka miwili mfululizo, 214 sawa na asilimia 88% walifukuzwa.

Watendaji wabovu wanagharimu pakubwa walipa kodi. Ndio maana nimependa kurejea uhusiano kati ya ufanisi wa Taasisi kwenye nafasi ya uchumi kwa kurejea Ripoti ya OxfordReview ya 2014, kwamba asilimia 25% ya uchumi wa mataifa13 makubwa zaidi kwa Uchumi Duniani, uchumi wao unatokana na ufanisi wa Taasisi ambao kwa kiasi kikubwa unategemea sana ubora wa rasilimali watu ikiwemo watumishi wa Umma..Ndio msingi wa hoja yangu kwetu wafanyakazi kuwa , Sheria inayotulinda dhidi ya uonevu isionee walipa kodi! 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad