JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TRFA Yaiomba Serikali Kudhibiti Tozo na Kuboresha Mazingira ya Sekta ya Usafirshaji

Share This

 


Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji wa Barabara wa Wizara ya Uchukuzi Andrew Magombana akizungumza wakati kufungua mkutano Mkuu wa Kwanza wa Chama cha Wasafirishaji wa Mizigo kwa Barabara Tanzania (TRFA) uliofanyika Hoteli ya Four Point Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi wa TRFA Vianey Rweyendela akizungumza kuhusiana na mikakati ya TRFA  katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa TRFA uliofanyika Hoteli ya Four Point  jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti waTRFA Sophia Caroline Mansoor akifunga mkutano mkuu wa Kwanza wa TRFA  uliofanyika Hoteli ya Four Point  jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TRFA Hussein Wandwi akitoa taarifa kwa Wanachama  katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa TRFA uliofanyika Hoteli ya Four Point  jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema imeanza kuchukua hatua za kutatua changamoto zinazokwamisha sekta ya usafirishaji nchini, ikiwemo msururu wa tozo unaowakabili wasafirishaji, foleni ya muda mrefu katika mpaka wa Tunduma na tozo za matumizi ya barabara zinazotozwa kwa madereva wa Tanzania nchini Zambia.

Hayo yamebainishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Chama cha Wasafirishaji wa Mizigo kwa Barabara Tanzania (TRFA) uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo wadau wa sekta hiyo waliwasilisha changamoto mbalimbali zinazoathiri uendeshaji wa biashara.

Akizungumza katika mkutano huo, Afisa Mtendadaji Mkuu wa TRFA Hussein Wandwi alisema kuwa moja ya changamoto kubwa ni tozo za barabara nchini Zambia ambazo zimeongeza gharama za uendeshaji kwa wasafirishaji wa Tanzania.

“Moja ya changamoto kubwa ni tozo mpya za barabara za Zambia. Kama wenzetu wanatoza malori yetu, nasi tunapaswa kuwatoza malori yao,” alisema Wandwi.

Alisema pia kuwa wasafirishaji wanakabiliwa na changamoto ya tozo kutoka Halmashauri na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), ikiwemo kodi ya huduma iliyopunguzwa kutoka asilimia 0.3 hadi 0.25 ya mauzo ya kila robo mwaka, ambayo bado inalalamikiwa na wadau.

Aidha, Wandwi aliitaka Serikali kuangalia upya mfumo wa mawakala wa usafirishaji wasio rasmi ili waweze kusajiliwa rasmi na kutambuliwa, sambamba na kusajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jambo litakalosaidia kuongeza uwazi na ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa TRFA Mkurugenzi Msaidizi wa Usafiri wa Barabara kutoka Wizara ya Uchukuzi, Andrew Magombana, alisema serikali imepokea malalamiko kuhusu tozo za Zambia na tayari imeanzisha mazungumzo na Serikali ya Zambia ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

Akizungumzia foleni katika mpaka wa Tunduma, Magombana alisema serikali za Tanzania na Zambia zinafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha mpaka huo unakuwa sehemu ya kupita badala ya kuwa sehemu ya kusubiri, huku hatua za kuongeza mageti zikitarajiwa kupunguza msongamano.

Naye Makamu Mwenyekiti wa TRFA, Sophia Caroline Mansoor, alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na serikali ili kutatua changamoto zilizopo, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya usafirishaji kwa kuwa Tanzania ni kitovu cha usafirishaji kwa nchi nyingi kupitia bandari zake.

Mansoor alisema kuboresha mazingira ya biashara katika sekta ya usafirishaji kutachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kuvutia uwekezaji zaidi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad