JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TRAMEPRO YASISITIZA UMUHIMU WA KULINDA URITHI WA MILA,UTAMADUNI NA TIBA ASILI

Share This

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO) limetoa limesisitiza kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda urithi wa mila, utamaduni, tiba asili na mazingira kama nguzo muhimu ya maendeleo endelevu ya Taifa.

TRAMEPRO inasisitiza kuwa maeneo ya mila, maarifa ya tiba asili, pamoja na mifumo ya jadi ya uhifadhi wa mazingira ni sehemu muhimu ya utambulisho wa jamii zetu. Taarifa iliyotolewa leo Aprili 17,2026 kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu

Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO) Boniventura Mwalongo,

   amesema kumekuwepo na changamoto za uvamizi wa maeneo ya mila, mabadiliko holela ya matumizi ya ardhi, pamoja na kuongezeka kwa upotoshaji wa dhana ya tiba asili.

“Mwito kwa Wazee na Machifu wa Mila

TRAMEPRO inatoa wito kwa viongozi wa mila kuendelea kusimamia kwa uaminifu maeneo ya jadi, kulinda urithi wa mababu, na kuendeleza maarifa ya tiba asili. Ushirikiano na Serikali na taasisi husika ni muhimu katika kuhakikisha amani na mshikamano wa kijamii unadumishwa.

Wito kwa Jamii kwa Ujumla

“Wananchi wote wanahimizwa kuthamini urithi wa kitamaduni, kuachana na imani potofu zinazokwamisha maendeleo, na kuzingatia sheria na miongozo rasmi. Umoja na uwajibikaji ni msingi wa ustawi wa Taifa.”

Aidha ametoa ombi kwa Serikali na Wadau wa Maendeleo kuviwezesha na kuviimarisha vikundi vinavyoendeleza tiba asili, utamaduni na uhifadhi wa mazingira, Kuimarisha ushirikiano wa tafiti kati ya taasisi za ndani na za kimataifa na Kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria za ardhi na utamaduni

Pia kuchukua hatua dhidi ya vitendo vinavyosababisha migogoro ya kijamii na uvunjifu wa amani.

“Nukuu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Kuhusu Mazingira na Utamaduni

“Tunapaswa kuthamini na kulinda mila zetu njema pamoja na mazingira yetu, kwa sababu hayo ndiyo msingi wa maendeleo endelevu ya Taifa letu.” 

“Pia Shirika linamkumbuka kiongozi mashuhuri wa dunia, Benjamin Franklin, aliyezaliwa tarehe 17 Aprili 1706. Alikuwa mfano wa maarifa, ubunifu na maadili mema, akisisitiza umuhimu wa elimu, nidhamu na hekima katika kujenga jamii imara,” amesema  Mwalongo,

Aidha amesema TRAMEPRO inawahimiza wananchi wote kushirikiana katika kulinda urithi wa utamaduni, kuendeleza tiba asili kwa misingi ya sayansi na teknolojia, pamoja na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad