JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TRA Yasisitiza Maadili kwa Watumishi, Wanaokiuka Kuchukuliwa Hatua

Share This

DAR ES SALAAM – Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema itaendelea kutoa elimu kwa watumishi wake kuhusu maadili ya kazi sambamba na kuchukua hatua kali dhidi ya wale watakaokiuka misingi ya utumishi wa umma.

Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa jukwaa la maadili la TRA, Kamishna Mwenda alisema mamlaka hiyo imejipanga kuhakikisha inaimarisha uwajibikaji na uadilifu ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Hafla hiyo imefanyika katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, na imewakutanisha watumishi mbalimbali wa TRA pamoja na wadau wa sekta ya mapato.

Kamishna Mwenda alisisitiza kuwa maadili ni msingi muhimu katika utendaji kazi wa TRA, akibainisha kuwa vitendo vya rushwa, uzembe au ukiukwaji wa taratibu havitavumiliwa.

Aliongeza kuwa utoaji wa elimu ya maadili utaendelea kufanyika mara kwa mara ili kuwajengea watumishi uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa jukwaa hilo wamesema mafunzo hayo ni muhimu katika kujenga taasisi imara yenye kuaminika kwa wananchi, huku wakiahidi kuzingatia maadili katika majukumu yao ya kila siku.




 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad