SHIRIKA la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO)limetoa ufafanuzi kuwa kwa mujibu wa taaluma ya afya na sayansi ya mwili wa binadamu, hakuna ushahidi wowote wa kitabibu unaothibitisha kuwa mwanaume anaweza kupoteza uume wake kwa kuguswa au kwa njia ya kichawi.
Ufafanuzi huo wa TRAMEPRO unakuja katika kipindi ambacho kumeibuka taarifa kuhusu kuongezeka kwa kasi kwa imani potofu, ushirikina na uzushi unaohusisha madai ya “kuguswa na kupoteza uume kwa wanaume” katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 6,2026 na Katibu Mkuu Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO) nchini Boniventura Mwalongo amesema kutokana na hali hiyo imeona ni vema ikatoa ufafanuzi katika hilo.
“Ukweli wa kisayansi na kitabibu kwa mujibu wa taaluma ya afya na sayansi ya mwili wa binadamu, hakuna ushahidi wowote wa kitabibu unaothibitisha kuwa mwanaume anaweza kupoteza uume wake kwa kuguswa au kwa njia ya kichawi.
“Matukio yanayoripotiwa mara nyingi huhusiana na hofu kali, mshtuko wa kisaikolojia na wasiwasi unaosababisha hisia zisizo sahihi mwilini.Mabadiliko ya muda mfupi ya mfumo wa fahamu au misuli.”
Amesema hivyo basi hiyo si tukio halisi la kimwili bali ni changamoto ya kisaikolojia inayohitaji uelewa sahihi na ushauri wa kitaalamu wa afya.
Hata hivyo amesema TRAMEPRO inaonya kuwa kuendelea kueneza taarifa zisizo na uthibitisho kunachochea hofu na taharuki katika jamii
Kunasababisha madhara kwa watu wasio na hatia.
“Kunadhoofisha juhudi za kukuza elimu ya afya na maendeleo ya jamii.Ni wajibu wa kila mwananchi kuepuka kusambaza uvumi na kuhakikisha taarifa zinathibitishwa kupitia vyanzo rasmi na sahihi.
Akifafanua zaidi amesema hatua hizo zinaendana na Kifungu cha (iii) cha Katiba ya TRAMEPRO kinachosema:
“(iii) Kupinga matumizi ya dawa asilia yanayopelekea na kuhamasisha vitendo vya jinai, mfano mauaji, wizi na vitendo vyote viovu.”
Pia amesema athari kwa jamii ni kuenea kwa imani hizo potofu kuna madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kuvuruga amani na mshikamano wa kijamii,kusababisha msongo wa mawazo na matatizo ya afya ya akili,kuwafanya wananchi kutumia rasilimali zao katika huduma zisizo sahihi pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa huduma stahiki za afya.
Mwalongo amesema TRAMEPRO inatoa mwito kwa wananchi wote kutafuta huduma za afya katika vituo rasmi pindi wanapopata dalili zisizo za kawaida,kupuuza na kupinga imani potofu zisizo na msingi wa kisayansi.
Poa kudumisha amani, utulivu na mshikamano katika jamii na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu vitendo vya utapeli au uchochezi wa uvunjifu wa amani
Wakati kwa vyombo vya habari vinahimizwa kutoa elimu sahihi kwa umma kwa kuzingatia weledi, ukweli na maadili ya taaluma ya habari,kuepuka kuripoti taarifa za uvumi bila uthibitisho pamoja na kushirikiana na wataalamu wa afya na taasisi husika katika utoaji wa taarifa sahihi.
Hata hivyo amesema TRAMEPRO inasisitiza mapambano dhidi ya imani potofu ni jukumu la wadau wote wa maendeleo na katika kuimarisha juhudi hizi iko tayari kushirikiana kwa karibu na
wadau mbambali ikiwemo Wizara ya Afya.
“Lengo ni kuhakikisha elimu sahihi kuhusu madhara ya uramali, urui, uzushi na ushirikina inawafikia wananchi wote, na vitendo hivi vinatambuliwa wazi kuwa ni hatari kwa ustawi wa jamii na vinapaswa kukemewa na kukomeshwa.”
“Ukweli wa kisayansi na kitabibu kwa mujibu wa taaluma ya afya na sayansi ya mwili wa binadamu, hakuna ushahidi wowote wa kitabibu unaothibitisha kuwa mwanaume anaweza kupoteza uume wake kwa kuguswa au kwa njia ya kichawi.
“Matukio yanayoripotiwa mara nyingi huhusiana na hofu kali, mshtuko wa kisaikolojia na wasiwasi unaosababisha hisia zisizo sahihi mwilini.Mabadiliko ya muda mfupi ya mfumo wa fahamu au misuli.”
Amesema hivyo basi hiyo si tukio halisi la kimwili bali ni changamoto ya kisaikolojia inayohitaji uelewa sahihi na ushauri wa kitaalamu wa afya.
Hata hivyo amesema TRAMEPRO inaonya kuwa kuendelea kueneza taarifa zisizo na uthibitisho kunachochea hofu na taharuki katika jamii
Kunasababisha madhara kwa watu wasio na hatia.
“Kunadhoofisha juhudi za kukuza elimu ya afya na maendeleo ya jamii.Ni wajibu wa kila mwananchi kuepuka kusambaza uvumi na kuhakikisha taarifa zinathibitishwa kupitia vyanzo rasmi na sahihi.
Akifafanua zaidi amesema hatua hizo zinaendana na Kifungu cha (iii) cha Katiba ya TRAMEPRO kinachosema:
“(iii) Kupinga matumizi ya dawa asilia yanayopelekea na kuhamasisha vitendo vya jinai, mfano mauaji, wizi na vitendo vyote viovu.”
Pia amesema athari kwa jamii ni kuenea kwa imani hizo potofu kuna madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kuvuruga amani na mshikamano wa kijamii,kusababisha msongo wa mawazo na matatizo ya afya ya akili,kuwafanya wananchi kutumia rasilimali zao katika huduma zisizo sahihi pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa huduma stahiki za afya.
Mwalongo amesema TRAMEPRO inatoa mwito kwa wananchi wote kutafuta huduma za afya katika vituo rasmi pindi wanapopata dalili zisizo za kawaida,kupuuza na kupinga imani potofu zisizo na msingi wa kisayansi.Poa kudumisha amani, utulivu na mshikamano katika jamii na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu vitendo vya utapeli au uchochezi wa uvunjifu wa amani
Wakati kwa vyombo vya habari vinahimizwa kutoa elimu sahihi kwa umma kwa kuzingatia weledi, ukweli na maadili ya taaluma ya habari,kuepuka kuripoti taarifa za uvumi bila uthibitisho pamoja na kushirikiana na wataalamu wa afya na taasisi husika katika utoaji wa taarifa sahihi.
Hata hivyo amesema TRAMEPRO inasisitiza mapambano dhidi ya imani potofu ni jukumu la wadau wote wa maendeleo na katika kuimarisha juhudi hizi iko tayari kushirikiana kwa karibu na
wadau mbambali ikiwemo Wizara ya Afya.
“Lengo ni kuhakikisha elimu sahihi kuhusu madhara ya uramali, urui, uzushi na ushirikina inawafikia wananchi wote, na vitendo hivi vinatambuliwa wazi kuwa ni hatari kwa ustawi wa jamii na vinapaswa kukemewa na kukomeshwa.”

No comments:
Post a Comment