Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. David Nchimbi alipokuwa akizinduwa kituo cha 'Kijitonyama FTTx Experience Center', kinacholenga kusambaza huduma ya intaneti yenye kasi, uhakika na bora katika makazi, ofisi, na maeneo ya biashara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. David Nchimbi (kulia) akizindua kituo cha 'Kijitonyama FTTx Experience Center', kinacholenga kusambaza huduma ya intaneti yenye kasi, uhakika na bora katika makazi, ofisi, na maeneo ya biashara. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa akishiriki uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. David Nchimbi (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha 'Kijitonyama FTTx Experience Center', kinacholenga kusambaza huduma ya intaneti yenye kasi, uhakika na bora katika makazi, ofisi, na maeneo ya biashara. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa akishiriki uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. David Nchimbi pamoja na viongozi mbalimbali wakitembelea maonesho ya bidhaa anuai ndani ya kituo cha 'Kijitonyama FTTx Experience Center', kinacholenga kusambaza huduma ya intaneti yenye kasi, uhakika na bora katika makazi, ofisi, na maeneo ya biashara.
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezinduwa kituo muhimu ambacho kimekuja kuendeleza mageuzi ya kidijitali nchini, kinachojulikana kama 'Kijitonyama FTTx Experience Center'. Kituo hicho bora na cha kipekee kimekuja kutoa uzoefu pamoja na elimu kuhusu matumizi ya teknolojia za kidijitali.
Akizungumza alipokuwa akizinduwa kituo hicho, leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Bw. David Nchimbi alisema mradi wa kituo cha FTTX unalenga kusambaza huduma ya intaneti yenye kasi, uhakika na bora katika makazi, ofisi, na maeneo ya biashara.
Aidha alisema kupitia kituo cha FTTX, wananchi wataweza kujionea kwa vitendo namna ambavyo intaneti ya TTCL
inavyoweza kubadilisha nyumba, ofisi au biashara kuwa za kidijitali na zenye ufanisi zaidi. Kituo hicho pia kitakuwa jukwaa la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi ya teknolojia za kisasa nyumbani, mifumo ya ofisi za kidijitali na suluhisho za biashara mtandao.
"...Ni dhahiri kuwa maisha ya sasa yanahitaji intaneti yenye kasi na uhakika, inayowezesha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kila siku—ikiwemo elimu mtandao, biashara mtandao, huduma za kifedha na mawasiliano ya haraka na yenye tija. Hivyo basi, ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunatumia fursa hizi za kidijitali kwa maendeleo ya taifa letu," alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Bw. Nchimbi.
Hata hivyo, aliupongeza uongozi wa Shirika la TTCL kwa kuendelea na Mkakati wa Mabadiliko ya kujiendesha biashara ikiwa pamoja na kutengeneza faida ya shilingi bilioni 22.9 (kabla ya kodi) katika mwaka wa fedha 2024/25, kwani mafanikio hayo yanatoa wajibu wa kuhakikisha shirika linaongeza mapato na kudumisha faida endelevu kupitia ufanisi, ubunifu na usimamizi madhubuti wa rasilimali za Shirika.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa akizungumza alibainisha kuwa TTCL inaendelea na Mpango Mkakati wa Kibiashara wa miaka 10, ambao utekelezaji wake umeanza katika mwaka wa fedha 2025/26, Mpango unaolenga kuleta mageuzi makubwa ndani ya shirika, hususan katika kuimarisha uwajibikaji, kuongeza uzalishaji wenye tija, na kuhakikisha uendelevu wa shughuli zetu.
"Katika mageuzi haya yanayoendelea, mojawapo ya hatua muhimu ni utekelezaji wa mradi wa Faiba - Fiber To The X (FTTx). Mradi huu unalenga kusambaza huduma ya intaneti yenye kasi, uhakika na bora katika makazi, ofisi, na maeneo ya biashara.
"Kupitia huduma ya “Faiba Mlangoni Kwako,” shirika linaendelea kupanua huduma hizi katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Unguja na mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mwanza, Geita, Iringa na Mbeya. Aidha, Shirika katika mwaka wa fedha 2026/27 limepanga kufikisha huduma hii ya Faiba katika mikoa iliyobakia nchini.' Alisisitiza Bw. Marwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa akizungumza katika uzinduzi wa kituo hocho, ambapo alibainisha kuwa TTCL inaendelea na Mpango Mkakati wa Kibiashara wa miaka 10, ambao utekelezaji wake umeanza katika mwaka wa fedha 2025/26, Mpango unaolenga kuleta mageuzi makubwa ndani ya shirika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Bw. David Nchimbi alisema mradi wa kituo cha FTTX.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Bw. David Nchimbi akitembelea maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazotolewa ndani ya kituo cha FTTX.


No comments:
Post a Comment