JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI, MHE. AMWAMBENE AZINDUWA MAADHIMISHO JUMA LA ELIMU (GAWE) 2026

Share This

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akihutubia wadau kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa 2026, - GAWE 2026, linalofanyika mkoani Songwe Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Juma la Elimu Kitaifa 2026.

Naibu Katibu Mkuu Elimu – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Atupele Mwambene akizungumza kwenye uzinduzi wa Juma la Elimu Kitaifa - GAWE 2026, linalofanyika mkoani Songwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika Juma la Elimu Kitaifa 2026, kabla ya kuzinduwa rasmi maonesho hayo.

NAIBU Katibu Mkuu Elimu – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Atupele Mwambene amezinduwa Juma la Elimu Kitaifa - GAWE 2026, linalofanyika mkoani Songwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba, akizungumza na wadau wa elimu kwenye hafla ya ufunguzi amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na wadau wa elimu katika kukuza sekta ya elimu nchini.

Mhe. Mwambene ameupongeza Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwa kuratibu maadhimisho haya na kuendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha wadau katika kujadili masuala ya msingi ya elimu bora, jumuishi na yenye usawa. Amebainisha kuwa GAWE 2026 ni jukwaa muhimu linalokuja wakati muafaka ambapo sekta ya elimu inahitaji mikakati madhubuti ya ndani kufuatia kupungua kwa misaada ya kimataifa.

Akizungumzia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Uhamasishaji wa Rasilimali za Ndani kwa Elimu Jumuishi, Bora na yenye Kuzingatia Mahitaji Maalum,” amesisitiza kuwa ni wajibu wa nchi kuimarisha mifumo ya ndani ya kugharamia elimu, kuongeza uwajibikaji na kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na usawa ili kufikia malengo ya elimu kwa wote.

Ameeleza kuwa GAWE 2026 kufanyika Mkoa wa Songwe, hususan Wilaya ya Momba, umetokana na uwepo wa changamoto mbalimbali za elimu ikiwemo upungufu wa walimu, miundombinu duni, viwango vya juu vya mdondoko wa wanafunzi pamoja na changamoto za kijamii kama mimba za utotoni.

Hata hivyo ametoa wito kwa wadau wote, serikali, jamii, sekta binafsi na asasi za kiraia, kuongeza uwekezaji na uwajibikaji katika elimu, na hatimaye kutangaza rasmi ufunguzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2026.

Awali kabla ya kuzinduwa, Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, alitembelea mabanda ya maonesho katika Juma la Elimu Kitaifa 2026 na kujionea kazi nzuri zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kutekeleza afua zinazolenga kuleta maendeleo ya jamii kupitia sekta ya elimu nchini Tanzania.

Mhe. Mwambene amefurahishwa na jitihada hizo, akisisitiza utayari wa Serikali kuendelea kushirikiana na wadau ili kufikia watu wengi zaidi. Aidha, amewahimiza wadau kuendeleza kazi hizo muhimu kwa ustawi wa taifa.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Juma la Elimu Kitaifa 2026, ametoa shukrani za dhati kwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI pamoja na uongozi wa Mkoa wa Songwe na Halmashauri ya Wilaya ya Momba kwa kuruhusu na kushirikiana katika maandalizi ya maadhimisho haya. Amepongeza mapokezi mazuri na ushirikiano mkubwa uliowezesha kufanyika kwa GAWE 2026 mkoani humo.

Ameeleza kuwa maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE 2026) yanayoanza leo, Aprili 20 hadi 24 ni jukwaa muhimu linalowaunganisha wadau wa elimu kitaifa na kimataifa kwa zaidi ya miaka 18, likiwa na lengo la kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora, jumuishi na yenye usawa. Mwaka huu, maadhimisho yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Uhamasishaji wa Rasilimali za Ndani kwa Elimu Jumuishi, Bora na yenye Kuzingatia Mahitaji Maalum,” ikilenga kuongeza uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa rasilimali za ndani kufuatia kupungua kwa misaada ya kimataifa katika sekta ya elimu.

Aidha, amebainisha kuwa zaidi ya mashirika 66 yameshiriki, yakiwemo wanachama 48 wa TEN/MET, yakishirikiana na serikali kukabiliana na changamoto za elimu hususan mkoani Songwe, ikiwemo upungufu wa walimu, miundombinu duni, mdondoko wa wanafunzi na mimba za utotoni. Kupitia GAWE 2026, juhudi zinaelekezwa katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, kuimarisha lishe shuleni, kuhamasisha urejeaji wa wanafunzi shuleni, pamoja na kuhakikisha rasilimali za elimu zinapatikana, zinagawanywa kwa usawa na kusimamiwa kwa uwazi kwa maendeleo endelevu ya sekta ya elimu nchini.

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika Juma la Elimu Kitaifa 2026, kabla ya kuzinduwa rasmi maonesho hayo.

Sehemu ya Washiriki wa Juma la Elimu Kitaifa - GAWE 2026, linalofanyika mkoani Songwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika Juma la Elimu Kitaifa 2026, kabla ya kuzinduwa rasmi maonesho hayo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Uchechemuzi wa Shirika la Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi (kushoto) akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI alipotembelea banda la shirika hilo kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2026, linalofanyika mkoani Songwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika Juma la Elimu Kitaifa 2026, kabla ya kuzinduwa rasmi maonesho hayo.

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika Juma la Elimu Kitaifa 2026, kabla ya kuzinduwa rasmi maonesho hayo.

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika Juma la Elimu Kitaifa 2026, kabla ya kuzinduwa rasmi maonesho hayo.

Mgeni rasmi wa siku ya ufunguzi, Mhe. Atupele Mwambene, Naibu Katibu Mkuu - Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akipata maelezo ndani ya Banda la Room to Read Tanzania kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2026, mkoani Songwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Maandamano ya wanafunzi kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2026, mkoani Songwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Maandamano ya wanafunzi kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2026, mkoani Songwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad