JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Kafulila: Muungano ni Watu Sio tu Serikali

Share This

 


MKURUGENZI wa Kituo Cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) David Kafulila amesema Muungano wa Tanzania ni wa kipekee barani Afrika kwa kuwa umejengwa juu ya misingi ya watu, na si serikali pekee.

Kupitia ukurasa wake wa X, Kafulila amesema Tanzania inaadhimisha miaka 62 ya Muungano ambao ni wa mataifa mawili huru barani Afrika uliofanikiwa kudumu kwa zaidi ya miongo sita.

Alitolea mifano ya miungano mingine barani Afrika iliyovunjika ndani ya muda mfupi, ikiwemo ule wa Ethiopia na Eritrea (1952-1962), Ghana-Guinea-Mali (1958-1963), na Senegambia (1982-1989).

Siri ya Mafanikio: Udugu na Utamaduni
Kafulila alieleza kuwa tofauti na miungano mingi ya Ulaya kama Umoja wa Ulaya au ya Asia ambayo inategemea zaidi makubaliano ya kiuchumi na kibiashara, Muungano wa Tanzania ulijengwa juu ya misingi imara ya udugu wa damu, lugha ya Kiswahili, na historia ya pamoja ya kijamii.

Jambo hilo, alisema, linaoufanya Muungano wa Tanzania kuwa na umoja wa watu zaidi kuliko umoja wa serikali pekee.

Alimalizia ujumbe wake kwa kusema: Tutazidi kuwakumbuka Nyerere na Karume siku zote kama hii.

Ujumbe huo umechapishwa ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa Aprili 26, 1964.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad