JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Upendo na Mshikamano miongoni mwa Wanawake FCC Utaongeza Ufanisi

Share This

Na Mwandishi Wetu

Wanawake wa Tume ya Ushindani (FCC ) wametakiwa kuwa na  upendo ambao utajenga mshikamano na kuleta ufanisi katika Taasisi.

Hayo ameyasema Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Magdarena Utouh katika  Maadhimisho  ya Siku ya  Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila Machi 8 ya kila mwaka.

Magdelena amesema maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni ishara ya kufanya wanawake  kuwa na  nguvu ambayo inatoa mchango katika Taifa pamoja na kuchochea maendeleo.

Amesema kuwa maadhimisho hayo ni pamoja ya kupeleka ujumbe kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa tuko nyuma yake na tunapiga kazi.

Aidha amesema.kuwa wanawake ni jeshi kubwa hivyo tunahitaji  kuendelea kujituma na kuleta matokeo  katika maeneo yetu ya kazi.

Kauli mbiu ya mwaka ya  Maadhimisho  ya Siku ya Wanawake Duniani  2026 ni Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050.











 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad